Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Hassan Abbas akizungumza na wanamichezo wanawake (hawapo pichani) wakati akifungua kongamano la Tamasha la Michezo la Wanawake mapema hii leo katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Hassan Abbas (kulia) akizungumza na wanamichezo wanawake wakati akifungua kongamano la Tamasha la Michezo la Wanawake mapema hii leo katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Hassan Abbas (hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la Tamasha la Michezo la Wanawake mapema hii leo katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Wasanii toka Kundi la Tanzania House of Talent (THT) wakitoa burudani Wakati wa uifunguzi wa kongamano la Tamasha la Michezo la Wanawake mapema hii leo katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanamichezo wanawake wakimsikiliza wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Hassan Abbas (hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la Tamasha la Michezo la Wanawake mapema hii leo katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Picha na WSUM –Dar es Salaam
*********************
Na. WSUM – Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Hassan Abbas amewataka Wanawake nchini kujiamini na kushiriki katika Michezo mbalimbali kwani Michezo ni fursa ya kutoa ajira nchini.
Hayo yamesemmwa na Katibu Mkuu huyo wakati akifungua kongamano la Michezo kwa Wanawake linalojulikana kwa jina la Tanzanite Women Sports Festival mapema hii leo katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
“Tamasha hili limepewa jina la Tanzanite Women Sports Festival ikiwa ni kutambua thamani ya kito hiki kwani ni cha pekee na Duniani kote hakipatikani zaidi ya ardhi ya Tanzania, hivyo wanawake wa Tanzania ni wa kipekee na wanaweza wanatakiwa kujiamini kuwa wanaweza”, alisema Dkt. Abbas.
Aidha Dkt. Abbas ameongeza kuwa kupitia tamasha hili la Tanzanite Women Sports Festival wanawake wengi wenye vipaji wataibuliwa kupitia Michezo mbalimbali itakayo chezwa ikiwemo soka la miguu kwa wanawake, mpira wa kikapu ndondi pamoja na Michezo mingine mingi.
“Kupitia tamasha hili la siku tatu serikali ina imani kubwa kuwa vipaji vingi vitaibuliwa kupitia Michezo mbalimbali itakayochezwa”, alisema Dkt. Abbas.
Tamasha la Tanzanite Women Sports Festival linafanyika kwa mara ya kwanza na litashirikisha Michezo mbalimbali na litafunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan siku ya Jumamosi Septemba 18 katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.