***************************
Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Katika hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya wananchi wameshiriki kumuua mnyama anaye sadikika kuwa ni fisi katika eneo la mto mumbu matanda mtaa wa Chamaguha Manispaa ya Shinyanga na kugawa na viungo vyake ikiwemo damu,miguu,kichwa, ngozi na kisha kuondoka navyo kwa sababu zisizojulikana.
Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo wamesema fisi huyo amegongwa na gari majira ya samoja asubuhi na kushidwa kutembea baada ya kuvunjika miguu yake ya mbele hali iliyomlazimu aingie kwenye mtaro wa barabara kwa lengo la kujificha kabla ya kuuawa na wanachi.
Mwenyekiti wa mtaa huo HUSSEN KATAMBA amewatahadharisha wananchi kuwa makini hasa kwa watoto kutokana na wanyama aina ya fisi kuonekana katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Shinyanga.
Amesema wanyama hao tayari wamesababisha madhara katika baadhi ya maeneo hivyo wazazi wanapaswa kuwalinda watoto.
“Natoa tahadhari hasa sisi wazazi tusiwaluhusu watoto kutembea asubuhi sana au usimu kumtuma dukani tuwe makini kwa sababu hatujui huyo fisi atatokea lini na sangapi hasa kwa maeneo ya chamaguha kwa sababu siyo mara ya kwanza kuonekana fisi kwahiyo nawaomba sana wazazi tuchukue tahadhari hiyo” amesema Katamba.
Aidha ameiomba serikali kupitia viongozi wa mali ya siri kutafuta njia ya kuwapata hao wanyama kabla hawajaleta madhara kwa wananchi hasa watoto.
“Tunasikia kwenye vyombo vya habari fisi wanajeruhi watu na kusababisha vifo na kama wanaendelea kuonekana namna hii itabidi wahusika hasa mali ya siri wajaribu kuwasaka ili kujua wanakaa wapi kwa sababu hili eneo hatuna msitu sasa tunajiuliza hawa fisi wanakaa wapi”.