Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi – CUF, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba akiwakaribisha wawakilishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa walipotembelea katika Afisi za Makao Makuu ya Chama hicho zilizopo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CUF, Haroub Mohammed Shamis, Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Ndani toka ORPP, Peter Lyimo na Mkuu wa Sehemu ya Usajili, Muhidin Mapeyo.
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Ndani toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP), Perter Lyimo akionyesha nakala ya Kanuni za Fedha za Vyama vya Siasa za mwaka 2019 mbele ya viongozi wa Chama cha Wananchi – CUF wakati wa zoezi la uhakiki katika Ofisi za chama hicho leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CUF, Haroub Mohammed Shamis, Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Ndani toka ORPP, Peter Lyimo na Mkuu wa Sehemu ya Usajili, Muhidin Mapeyo.
Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi wa Chama cha Wananchi – CUF Taifam Bi. Zainab Mndolwa Amiri akielelezea jambo kuhusu matumizi ya hundi katika malipo yanayofanyika katika chama chao mbele ya Maafisa kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakati wa zoezi la uhakiki wa namna kinavyotekeleza matakwa ya Sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) leo jijini Dar es Salaaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi – CUF, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba akifafanua jambo mbele wawakilishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa walipotembelea katika Afisi za Makao Makuu ya Chama hicho zilizopo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya zoezi la uhakiki . Kutoka kushoto ni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Ndani toka ORPP, Peter Lyimo(katikati).
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza (katikati) akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wa kitaifa wa Chama cha Wananchi – CUF mara bada ya kumaliza zoezi la uhakiki kuhusu namna chama hicho kinavyotekeleza Sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) linaloendelea nchini.
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kitaifa wa Chama cha Wananchi – CUF mara bada ya kumaliza zoezi la uhakiki kuhusu namna chama hicho kinavyotekeleza Sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) linaloendelea nchini. (Picha na: ORPP)