Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akisalimiana na wananchi mara baada ya kuwasili katika maadhimisho ya epidemiolojia na maabara Duniani yaliyofanyika leo September 7,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akiwaangalia wananchi waliojitokeza kutoa Damu maadhimisho ya epidemiolojia na maabara Duniani yaliyofanyika leo September 7,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.Dorothy Gwajima,akisoma ujumbe uliopo katika bango wakati wa maadhimisho ya epidemiolojia na maabara Duniani yaliyofanyika leo September 7,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akizungumza wakati wa maadhimisho ya epidemiolojia na maabara Duniani yaliyofanyika leo September 7,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akisisitiza jambo wakati wa maadhimisho ya epidemiolojia na maabara Duniani yaliyofanyika leo September 7,2021 jijini Dodoma.
MKurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya Dkt.Leonard Subi,akizungumza wakati wa maadhimisho ya epidemiolojia na maabara Duniani yaliyofanyika leo September 7,2021 jijini Dodoma.
rais wa Umoja wa Field Epidemilojia Tanzania (TANFLEA) Dkt Elibariki Mwakapeje ,akizungumza wakati wa maadhimisho ya epidemiolojia na maabara Duniani yaliyofanyika leo September 7,2021 jijini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo ka Muhambwe (CCM) Dkt. Florence Samizi ,akizungumza wakati wa maadhimisho ya epidemiolojia na maabara Duniani yaliyofanyika leo September 7,2021 jijini Dodoma.
Wizara ya Mifugo na Uvuvi Idara ya Huduma za Mifugo Dkt.Justine Assenga,akizungumza wakati wa maadhimisho ya epidemiolojia na maabara Duniani yaliyofanyika leo September 7,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho ya epidemiolojia na maabara Duniani yaliyofanyika leo September 7,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Afya Mendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto Dkt Doroth Gwajima amesema kuwa matumizi ya takwimu zenye ubora katika halmashauri nchini bado ni changamoto hali ambayo inarudisha nyuma sekta ya afya.
Hayo ameyasema leo September 7,2021 wakati wa madhimisho ya siku ya Epidemiology Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere square Dkt.Gwajima amesema kuwa ili kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa na matukio yanayoathiri afya ni vema kutambua mapema viashiria hatari.
“Katika jamii yetu ni lazima pawepo na takwimu zenye ubora katika ngazi ya halmahauri jambo litakalo saidia kuinua sekta ya afya, ” amesema Dkt Gwajima
Aidha Dkt.Gwajima ameeleza kuwa jumla ya watumishi 512 kutoka idara ya afya ya binadamu na idara ya afya ya mifugo wamepatiwa mafunzo katika ngazi ya kozi ya awali kutoka mikoa yote 26 na halmashauri 159 kwa kipindi cha miaka sita.
Kwa upande wake rais wa Umoja wa Field Epidemilojia Tanzania (TANFLEA) Dkt Elibariki Mwakapeje amesema kuwa wao kama TANFLEA ni kuhakikisha afya ya mtanzania inaimarika ili watu waweze kuwa na afya bora ili aendelee kufanya shughuli zao za kila siku.
”Lengo la maadhimisho hayo ni namna ya kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza”amesema Mwakapeje
MKurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya Dkt.Leonard Subi amesema zaidi ya watanzania 512 wamepatiwa mafunzo ya utaalam wa epidemiolojia na maabara katika mikoa yote 26 Tanzania
Madhimisho ya siku ya Epidemiology yamefanyia kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kuadhimishwa siku ya wataalamu wa epidemiolojia na maabara ambao ndiyo makachero wa magonjwa yote ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza ili kutambua visababishi vya magonjwa na jinsi magonjwa yanavyo sambaa kwenye jamii .
Hata hivyo madhimisho hayo yamebebwa na kauli mbiu isemayo kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa na matukio yanayoathiri afya ili kutambua viashiria hatari kwa jamii.