Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi wakati alipoiwakilisha serikali katika mazishi ya Mke wa mwanasheria Mkuu wa Serikali, Natalia Bahati Kilangi yaliyofanyika Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza katika mazishi ya Natalia Bahati Kilangi, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi yaliyofanyika Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia kwa Waziri Mkuu) wakishiriki katika ibada ya mazishi ya Natalia Bahati Kilangi, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi yaliyoanyika Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. Wengine pichani kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana,Ajira, na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Waziri wa Madini, Doto Biteko. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Natalia Bahati Kilangi, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi katika mazishi yaliyofanyika Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitupa udongo kwenye kaburi la Natalia Bahati Kilangi, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi, katika mazishi yaliyofanyika Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Serikali, Profesa Adelardus Kilangi (wa pili kushoto) na familia yake wakishiriki katika Ibada ya mazishi ya Natalia Bahati Kilangi, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali yaliyofanyika Luchelele jijini Mwanaza Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye kaburi la Natalia Bahati Kilangi, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Profesa Kilangi, Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuui, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Renatus Nkwande na Askofu wa Jimbo la Geita, Flavian Kassala katika mazishi ya Natalia Bahati Kilangi, Mke wa mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi yaliyofanyika Luchelele jijini Mwanza, Agosti 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
*************
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo, Agosti 7, 2019 ameongoza mazishi ya mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi, Bibi Natalia Bahati Kilangi.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali katika mazishi hayo yaliyofanyika nyumbani kwa Profesa Kilangi eneo la Luchelele jijini Mwanza, Waziri Mkuu amemuomba Profesa Kilangi na familia yake kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu ambapo wamempoteza mama ambaye ni nguzo muhimu ya familia.
Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasilisha salamu za pole kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa Profesa Kilangi na familia yake kutokana na msiba mzito walioupata.
Katika salamu zake Rais Dkt. Magufuli amesema Serikali inathamini sana mchango mkubwa na mahili unaotolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na anamini kwamba kwa vyovyote vile wakati wa uhai wake, marehemu Natalia alishiriki kwa kiwango kikubwa kuhakikisha kwamba mumewe anaifanya kazi yake vizuri.
Awali, Spika wa Bunge, Job Ndugai aliwasihi waombolezaji wote wamkumbuke katika sala zao, Mwanasheria Mkuu wa Seriakali Profesa Kilangi ambaye ana kazi nzito ya kuishauri Serikali na alimtaja kuwa ni kiungo muhimu cha mihimili yote mitatu.
Naye, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Renatus Nkwande alimuomba Profesa Kilangi na familia yake wajipe moyo kwa sababu binadamu anapokuwa hai au anapokufa bado anabaki kuwa mali ya Mwenyezi Mungu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Mabenki nchini, Abdulmajid Msekela ambaye pia ni Mkurugenzi wa Benki ya CRDB alisema wanachama wote wa umoja huo wanatoa pole kwa familia na wanamwombea Mwanasheria Mkuu wa Serikali na familia nzima, Mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki cha majonzi.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria katika mazishi hayo ni pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Augustine Mahiga, Waziri wa Madini, Doto Biteko, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga.
Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ally, Manaibu Mawazi, Wakuu wa Mikoa na wilaya na viomgozi mbalimbali wa Serikali.
Mazishi hayo pia yalihudhuriwa na Askofu wa Jimbo la Geita na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania(TEC), Flavian Kassala, Mapadri na Masheikh kutoka maeneo mbalimbali nchini