Mkurugenzi wa Jumua ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) Jamila Mahmoud alipokia akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa mradi huo.
Picha ya pamoja ya viongozi wa wilaya pamoja na wahitimu hao wakiongozwa na wawakilishi wa ZAFELA pamoja na TAMWA-ZNZ.
***************************
Na Masanja Mabula
Mkuu wa Wilaya ya Magharib A Unguja Suzan Petar Kunambi amesema anaamini kuwa ifikapo mwaka 2030 Zanzibar tayari itakua na idadi kubwa ya viongozi wengi wanawake katika nafasi za juu Serikali na hata za kijamii, kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na Asasi nyengine visiwani visiwani hapa.
Akiyasema hayo wakati wa mkutano maalumu wa uzinduzi wa uhamasishaji wanawake kushiriki katika nafasi mbali mbali za uongozi ,mkutano umefanyika katika viwanja vya mnara wa kisonge.
Alisema wanawake wengi ni watu wenye uwezo mkubwa wa kuongoza wengine kuliko jamii inavyofikiria,na kwamba jamii hawana budi kuwaunga mkono wanawake katika maeneo yao hatimae waweze kuwa viongozi.
Akizungumzia kuhusu suala la uaminifu alisema wanawake pia ni watu waliojaliwa na tabia hiyo na kueleza kuwa ni miongoni mwa sifa muhimu ambazo viongozi wanapaswa kuwa nazo.
Sambamba na hayo Mkuu huyo wa Wilaya alisema kufanyika kwa mkutano huo wa uzinduzi ni kwenda sambamba na dira ya Serikali katika kuwajengea uwezo wanawake walio wengi kusimama kama viongozi kwenye Serikali au hata nje ya serikali.
Awali Mkururugenzi wa Jumuia ya Wanasheria wanawake Zanzibar (ZAFELA)Jamila Mahmoud alisema uzinduzi huo umekuja baada ya kupatikana kwa vijana 60 ambao waliwafanyia mafunzo maalumu ambao nao watakwenda kutoa mafunzo hayo katika maeneo yote ya Unguja.
Alisema vijana hao watafanya kazi kwa kila shehi za Mikoa yote ya Unguja huku lengo kuu likiwa ni kuijengea uwelewa jamii juu ya ushirikishwaji wa wanawake kwenye nafasi za uongozi ziwe za kiserikali au hata za kijamii.
Awali akizungumza kwa niaba ya vijana ambao wamehitimu mafunzo hayo Fransisca Claimant alisema mafunzo hayo yamewajengea uwezo mkubwa na wapo tayari kuyafanyia kazi na hatimae elimu hio kuifikia jamii.
Mradi wa uhamasishaji wanawake kushiriki nafasi za uongozi ni wa miaka mine na unatekelezwa na TAMWA-ZNZ,kwa kushirikiana na ZAFELA pamoja na PEGAO chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Norway Nchini Tanzania.