Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiongoza matembezi (mazoezi) yaliofanyika hii leo Septemba 4,2021 kuanzia viwanja vya Bunge kuelekea viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango pamoja na Wabunge, Viongozi mbalimbali na Watendaji wa benki ya NMB wakifanya mazoezi ya viungo katika viwanja vya Chinangali Dodoma mara baada ya kumalizika kwa matembezi (mazoezi) yalioanzia katika viwanja vya Bunge la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na washiriki waliojitokeza katika tamasha la kivumbi na Jasho lililoshirikisha Benki ya NMB na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika viwanja vya Chinangali Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwapokea msaada wa taulo za kike zilizotolewa na Benki ya NMB na kukabidhi kwa uongozi wa Mkoa wa Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika picha ya pamoja na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na uongozi wa Benki ya NMB wakati wa Tamasha la Kivumbi na Jasho lililoandaliwa na NMB kwa kushirikiana na Bunge.
……………………………………………………………………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango hii leo Septemba 4, 2021 ameshiriki Tamasha la NMB na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lenye kauli mbiu ya “Kivumbi na Jasho” lililofanyika jijini Dodoma. Tamasha hilo lililoratibiwa na Benki ya NMB linalenga kuchangia maendeleo katika sekta mbalimbali na kuanza katika sekta ya elimu mkoa wa Dodoma.
Aidha Makamu wa Rais ameongoza mazoezi ya matembezi yalioanzia katika viwanja vya Bunge kuelekea viwanja vya Chinangali mkoani Dodoma.
Akizungumza katika Tamasha hilo Makamu wa Rais ameipongeza Benki ya NMB kwa kuandaa tamasha hilo kwaajili ya afya za washiriki lakini pia uwepo wa dhima mbalilmbali katika kuandaa matamasha hayo unaolenga kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi. Amesema msaada wa vifaa vya kufundishia uliotolewa katika tamasha hilo utapunguza changamoto inazozikabili shule mbalimbali mkoani Dodoma.
Aidha amewasihi kuendelea na tamasha hilo katika maeneo mbalimbali ya nchi ili kuendelea kutatua changamoto katika sekta ya afya na elimu.
Makamu wa Rais amewataka watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya janga la Uviko 19 na kusema kwamba Tanzania bado inakabiliwa na Janga hilo hivyo njia mojawapo ya kupambana na ugonjwa huo ni kufanya mazoezi mara kwa mara.
Kwa upande wake Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson Mwansasu amesema Bunge litaendelea kushirikiana na NMB katika matamasha hayo na kuipongeza NMB kwa mpango wao wa muda mrefu waliouandaa unaolenga kuchangia wanawake waliopata changamoto ya Fistula hapa nchini.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Ruth Zaipuna ameishukuru serikali kwa jitihada zinazoendelea kuchukuliwa kupitia benki kuu kuhakikisha mikopo inatolewa kwa urahisi na riba kuendelea kushuka. Amesema Benki NMB itaendelea kushirikiana na Benki Kuu kuhakikisha malengo haya yanafikiwa kiurahisi.