BONDIA Hassan Mwakinyo amefanikiwa kutetea mkanda wake wa Chama cha Ngumi Afrika (ABU) baada ya ushindi wa Technical Knockout (TKO) raundi ya nne dhidi ya Mnamibia, Julius Indongo usiku wa Ijumaa ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Lakini mambo hayakuwa mazuri kwa Mtanzania mwingine, Tony Rashid kupigwa na Bongani Mahlangu wa Afrika Kusini kwa TKO raundi ya pili katika pambano la ABU pia uzito wa Super Bantam.