Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, Edward Mpogolo (wa pili kushoto) akikabidhi Pikipiki kwa mmoja wa watendaji wa kata wa Wilaya hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Yusto Mapande na watatu ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Same, Anastazia Tutuba.
Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, Edward Mpogolo akiwa amepanda moja ya Pikipiki ambazo amezikabidhi kwa watendaji wa Kata 16 kwenye Wilaya hiyo.
Baadhi ya Pikipiki ambazo Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, Edward Mpogolo amezikabidhi kwa watendaji 16 wa Wilaya hiyo.
Na Mwandishi Wetu, Same
MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Edward Mpogolo amewakabidhi Maafisa Watendaji wa Kata 16 pikipiki ili kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa miradi na kuhakikisha Halmashauri hiyo inafikia lengo walilojiwekea kwenye ukusanyaji wa mapato na utoaji wa huduma kwa Wananchi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi pikipiki hizo gawaji pikipiki hizo Mpogolo aliipongeza Halmashauri ya Same kwa kutenga fedha na kununua vitendea kazi hivyo kwa watendaji na kuahidi kuwa simamia watendaji hao kuzitumia pikipiki hizo kama ilivyokusudiwa
na si vinginevyo.
Mpogolo alisema watendaji waliokabidhiwa pikipiki hizo wahakikishe wanajifunza kuendesha na kupata leseni, na kuwa hatamfumbia macho mtendaji yeyote atakaye badilisha matumizi yake.
“Ni kweli wenzetu wa Halmashauri wametoa fedha kwa ajili ya kununua pikipiki hizi kwa watendaji wetu wa Kata 16, lengo ni kufikia kata zote 34 na kuifanya halmashauri yetu kuwa ya mfano wa kusimamia maendeleo na kutoa huduma kwa wananchi wa Same,”. “alisema Mpogolo.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Annastazia Tutuba akitoa taarifa ya ununuzi wa pikipiki hizo alisema wametumia kiasi cha Sh. 43.6 milioni kununua pikipiki hizo 16 na katika pesa hizo kiasi cha Sh.Milioni 6 zimetumika kununua pikipiki ya magurudumu matatu (Guta) kwa ajili ya shughuli mbalimbali za mamlaka ya mji mdogo wa Same.
Tutuba alisema lengo la Halmashauri ni kuwajengea mazingira rafiki ya ukusanyaji wa mapato watendaji wake wa kata ili kuongeza ufanisi na kufikia malengo waliyojiwekea ya ukusanyaji wa mapato ya Sh. Bilioni 2.5 kwa mwaka wa fedha 2021-2022.
“Tumeona ni vyema kuwanunulia pikipiki watendaji wetu hawa wa Kata 16 ili kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato kwenye kata zao na ukiangalia kata tulizopeleka pikipiki hizi ni zile zenye changamoto ya usafiri na nyingi ni za milimani,” alisema Tutuba