Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani akiwahutubia wakulima leo wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Usambazaji wa Teknolojia ya Kilimo cha Kanda ya Magharibi kilichopo chini ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI-Tumbi)
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (katikati) akikata utepe kuzindua leo Kituo cha Usambazaji wa Teknolojia ya Kilimo cha Kanda ya Magharibi kilichopo chini ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI-Tumbi)
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani akikagua leo mbegu ya alizeti aina ya Rekodi inazalishwa na Kituo cha Usambazaji wa Teknolojia ya Kilimo cha Kanda ya Magharibi kilichopo chini ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI-Tumbi)
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Nawanda akitoa maelezo ya utangulizi leo wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Usambazaji wa Teknolojia ya Kilimo cha Kanda ya Magharibi kilichopo chini ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI-Tumbi)
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI) Richard Kasuga akitoa maelezo ya Taasisi hiyo leo kabla ya uzinduzi wa Kituo cha Usambazaji wa Teknolojia ya Kilimo cha Kanda ya Magharibi
Picha na Tiganya Vincent
**********************************
NA TIGANYA VINCENT
KILA Halmashauri Mkoani Tabora imeagizwa kupeleka Maafisa Ugani 100 na baadhi ya wakulima katika Kituo cha Usambazaji wa Teknolojia ya Kilimo cha Kanda ya Magharibi ili wapate elimu itakayowasaidia kutoa huduma zitakazoongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani wakati akizundua Kituo cha Usambazaji wa Teknolojia ya Kilimo cha Kanda ya Magharibi kilichopo chini ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI-Tumbi)
Alisema Maafisa Ugani wanapaswa kuwa elimu ya kisasa ya kuwafanya wakulima wakulima kuongeza uzalishaji na kuinua hali za maisha yao na Halmashauri za Wilaya kuongeza mapato yao.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka TARI –Tumbi kusaidia uzalishaji wa mbegu za mazao mbalimbali ambayo hayalimwi na yanaweza kustawi mkoani humo kwa ajili ya kuwawezesha wakulima kulima mazao mengi.
Katibu wa Chama cha Mainduzi(CCM) Mkoa wa Tabora Solomon Kasaba alikipongeza Kituo cha Utafiti wa Kilimo Tanzania kwa kupiga hatua ya kuanzisha Kituo hicho mkoani humo ambacho ni muhimu katika kuleta mapinduzi ya kilimo.
Aliwataka kuangalia uwezekano wa kutumia Kituo kupeleka huduma za Teknolojia ya Kilimo katika maeneo wanayoishi wakulima wengine ili waondokane na kilimo kwa ajili ya kujikimu na kuingia katika kilimo cha kibiashara ambacho ndio kitasaidia kuwainua kichumi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tabora Dkt.Yahya Nawanda alisema kuwa wanatarajia kutumia fursa ya uwepo wa Kituo hicho kupeleka Maafisa Ugani kwa ajili ya kujifunza na baada ya hapo watapeleka elimu hiyo kwa wakulima.
Alisema hatua hiyo itasaidia kuwawezesha kulima kilimo cha aina mbalimbali ikiwemo cha bustani kwa maarifa ya kisasa
Kwa upande wa Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI) Richard Kasuga alisema wamejipanga kuhakikisha kuwa Kituo cha Usambazaji wa Teknolojia ya Kilimo cha Kanda ya Magharibi kinawasaidia wakulima kupata elimu itakawasaidia kuzalisha kwa tija