Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kwimba, Chuki Anthony akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM. Dk. Bashiru Ally alipowasili wilayani humo juzi.
Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally (wa pili kutoka kushoto), akishiriki kuimba wimbo na wana CCM wilayani Kwimba (hawapo pichani) katika Kata ya Hungulamalwa juzi.
Mmoja wa wanachama wapya waliojiunga na CCM ambaye jina halikufahamika mara moja akivishwa kofia na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally wilayani Kwimba.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Dk. Anthony Diallo akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu za Wilaya,Kata na Matawi pamoja na wajumbe wa mabaraza ya jumuiya za Chama wilayani Kwimba juzi kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Dk. Bashiru Ally.
Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally akiwahutubia wajumbe wa Halmashauri Kuu za Wilaya,Kata na Matawi pamoja na wajumbe wa mabaraza ya jumuiya za Chama wilayani Kwimba juzi
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally (wa nne kutoka kulia) akikata utepe kuzindua Tawi la Nyambogo la Wakereketwa wa CCM wilayani Kwimba juzi.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ally, akifunga kamba baada ya kupandisha bendera ya Chama muda mfupi mara baada ya kuzindua tawi la Nyambogo la wakereketwa wa CCM wilayani Kwimba juzi.
Picha zote na Baltazar Mashaka.