********************************
Na Mwandishi wetu, Mirerani
Uongozi wa Masjid Irishaad wa Songambele Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, umewaomba wadau wa maendeleo nchini kujitolea fedha kiasi cha shilingi milioni 22 ili kukamilisha upauzi wa msikiti wao.
Imamu wa msikiti huo Yusuph Said ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya gharama za upauzi wa msikiti huo akiomba wadau wajitokeze kusaidia.
Imamu Yusuph amesema wadau wa maendeleo nchini na nje ya nchi wanaalikwa kuchangia ujenzi wa msikiti huo ili wawe ni miongoni mwa wanaotarajiwa kupata herina Mwenyezi Mungu atawalipa.
Amesema msikiti ni eneo ambalo linabadili maisha ya watu kwa sababu matendo ya wema na kumcha Mungu ndiyo yanayofanyika hivyo wenye uwezo wanapaswa kuchangia chochote walichojaliwa.
“Wadau wote wa maendeleo nchini ambao Mwenyezi Mungu amewajalia tunaomba washiriki kutuchangia fedha walizojaliwa ili tuweze kukamilisha ujenzi wa msikiti wetu,” amesema Imamu Yusuph.
Katibu wa Masjid Irishaad Songambele, Ally Msuya amesema uongozi wa msikiti huo, unapokea fedha na vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kukamilisha upauzi wa msikiti huo.
Msuya amesema hatua nyingine za umaliziaji wa jengo lote la msikiti huo watatoa tathimini siku za karibuni kadiri ujenzi wake utakavyoendelea katika hatua mbalimbali.
Amesema gharama za ujenzi huo utajumuisha misumari kilo 100 ya gharama ya shilingi 600,000 bati 1,494 za gauge 28 shilingi 19,720,800 na gharama za fundi shilingi milioni 2.
Imamu msaidizi wa Masjid Irishaad Songambele, Khalifa Issa amesema wadau wa maendeleo wanaweza pia kuchangia kupitia akaunti ya benki ya NMB iliyofunguliwa.
Khalifa ametaja nambari ya akaunti ya ujenzi wa msikiti huo kuwa ni Benki ya NMB 43010003187 hivyo wadau wenye kupenda kuchangia kupitia benki wanaomba kufanya hivyo.
Amesema mdau anayependa kuchangia ujenzi wa msikiti huo anaweza kuwasiliana na Imamu wa msikiti huo Said kupitia namba za simu 0753757313 na Katibu wa Msikiti huo Ally Msuya namba za simu 0755505931.