Kikao kazi cha wadau wa
Sekta ya Afya kimeanza leo jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Seascape,
kikikuhusisha wataalamu katika masuala ya Uhakiki Ubora, Usalama wa Afya na Kujiandaa
na Magonjwa ya Mlipuko. Kikao hicho kimelenga kujadili masuala na changamoto
mbalimbali katika sekta hiyo na kupendekeza hatua za kuchukua ili kuongeza tija
na ubora katika utoaji wa Huduma za Afya nchini kupitia wadau ikiwemo Sekta
Binafsi.
Akizungumza wakati wa
kufungua kikao hicho, Dkt. Eliudi S. Eliakimu, Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa
Huduma za Afya kwa niaba ya Wizara ya Afya, amesema mkutano huo ni muhimu kwa
wadau wa afya kujadili changamoto mbalimbali zinazohusu ubora na usalama wa
huduma za Afya, na kwamba kupitia mkutano huo Wizara imekuwa inapokea mrejesho
na kupokea mapendekezo mbalimbali ya wadau kuhusu kuboresha utoaji wa huduma za
Afya, pamoja na kukubaliana hatua za kuchukua ili kuongeza ubora wa huduma na
udhibiti wa magonjwa.
“ Pamoja na kukabiliwa
na changamoto mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa UVIKO – 19 uliosababisha wadau
kutokutana kwa muda mrefu, tunashukuru Chuo Kikuu Mzumbe, kupitia mradi wa CDC –
PEPFAR waliofadhili mkutano huu muhimu kwa wadau, ambao baadhi ya wadau wengine
wameweza kushiriki kwa njia ya mtandao”. Alisema
Akizungumza kwa niaba
ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Henry A. Mollel Mratibu na msimamizi
wa mradi wa CDC – PEPFAR amesema “Chuo Kikuu Mzumbe kitaendelea kushirikiana
kwa karibu na Wizara ya afya kuboresha mifumo ya afya nchini, kupitia wataalamu
wake waliopo kwenye Kituo Bora cha Ufuatiliaji na Tathmini ya Mifumo na Miradi
ya Afya, chini ya Skuli ya Utawala wa Umma na Menejimenti, pamoja na kuendelea
kufadhili mikutano ya wadau wa Afya, chini ya mradi wa CDC – PEPFAR.
Wakizungumza kwa
nyakati tofauti washiriki wa mkutano huo wameshukuru Chuo Kikuu Mzumbe kwa
kuwezesha kikao hicho kufanyika, kutokana na mahitaji makubwa yaliyopo kwa sasa
kwenye Sekta ya Afya, ambayo yanahitaji majadiliano na makubaliano ya pamoja,
ambayo yatatoa mjumuisho na fursa ya kurekebisha masuala mengi ya kisekta,
pamoja na kuongeza ubora katika udhibiti, uhakiki na ukaguzi wa mifumo
mbalimbali ya utoaji huduma za Afya nchini.
Zaidi ya washiriki
thelathini wameshiriki kitika kikao hicho na wengine 20 wameshiriki kwa njia ya
mtandao, kutoka Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais TAMISEMI, wawakilishi kutoka shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), Kituo cha
Udhibiti wa Magonjwa (CDC), Taasisi ya Taifa ya Utafiti na Tiba (NIMR), USAID,
AMREF, UNICEF, GTZ, CSSC, Engender, MDH, AGPAHI, Pharmaccess, EGPAF, Chuo Kikuu
Mzumbe na wengineo. Kikao kazi hiki
kimefanyika kwa mara ya kwanza tangu kilipofanyika kwa mara ya mwisho miaka
miwili iliyopita, kutokana na changamoto za rasilimali na ugonjwa wa UVIKO – 19.
Eliakimu akizumgumza na wadau mbalimbali Sekta ya Afya wakati akifungua kikao kazi
cha wadau wa Sekta ya hiyo leo Agosti
26, 2021. jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Hoteli ya Seascape.Mratibu na Msimamizi wa Mradi wa CDC – PEPFAR kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Henry A. Mollel akizumgumza
na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya juu kuendelea kushirikiana kwa karibu na Wizara ya afya ili kuboresha mifumo ya afya nchini wakati wa kufungua kikao kazi cha wadau wa
Sekta ya hiyo leo Agosti 26,
2021. jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Hoteli ya Seascape.Mratibu na Msimamizi wa Mradi wa CDC – PEPFAR kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Henry A. Mollel (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya,Dkt. Eliudi S. Eliakimu wakati wa kufungua kikao kazi cha wadau wa Sekta ya Afya leo Agosti 26, 2021. jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Hoteli ya Seascape.
ya wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa
Huduma za Afya,Dkt. Eliudi S. Eliakimu (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha wadau wa
Sekta ya hiyo leo Agosti 26, 2021. jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Hoteli ya Seascape.
ya Afya leo Agosti 26, 2021. jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Hoteli ya Seascape. (Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)