MKUU wa Mkoa wa Dodoma ,Anthony Mtaka,akizungumza wakati wa hafla ya kupokea mabomba kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa malipo kwa matokea awamu ya nne Kimkoa ilifanyika Jijini Dodoma.
Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini ,Anthony Mavunde,akizungumza wakati wa hafla ya kupokea mabomba kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa malipo kwa matokea awamu ya nne Kimkoa ilifanyika Jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ,Anthony Mtaka,(hayupo pichani) wakati wa hafla ya kupokea mabomba kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa malipo kwa matokea awamu ya nne Kimkoa ilifanyika Jijini Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma ,Anthony Mtaka,akikata utepe wakati wa hafla ya kupokea mabomba kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa malipo kwa matokea awamu ya nne Kimkoa ilifanyika Jijini Dodoma.
…………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Dodoma ,Anthony Mtaka ametoa muda wa miezi mitatu kwa Wakala wa maji safi na mazingira Vijijini (RUWASA) kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa miradi ya maji mkoani Dodoma.
Kauli hiyo ameitoa jijini Dodoma wakati wa hafla ya kupokea mabomba kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa malipo kwa matokea awamu ya nne Kimkoa.
RC Mtaka amewataka RUWASA kuhakikisha wanauwaunganishia maji wananchi wa maeneo yote yaliyopo kwenye mpango huo ndani ya muda wa miezi mitatu vinginevyo watawajibishwa kisheria .
“Takukuru wapo hapa na Jeshi la Polisi wapo hapa ,Sisi tumealikwa kwa nia njema kabisa kuja kushuhudia kazi hii nzuri ,sasa baada ya miezi mitatu hawa ambao umewakaribisha kuja kushuhudia hafla hii watageuka sasa kuanza kuwashughulikia ninyi kama mkishindwa ,sijui kama ninaeleweka ”amesema Mtaka .
Hata hivyo ameeleza kuwa lengo la kutoa vifaa hivyo ni kuondoa tatizo la maji maeneo hayo ambalo limekuwa la muda mrefu hivyo nia njema hiyo isiharibiwe na watendaji wachache wazembe .
Aidha ameielekeza RUWASA kuhakikisha vifaa vyote vilivyotolewa kwa ajili ya mradi huo kupelekwa Wilaya husika pamoja na Vijijji kuhakikisha haraka ili kuwafikishia walengwa huduma hiyo ya maji .
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa maradi huo Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Dodoma ,Dk.Godfrey Mbabaye amesema kuwa mambomba hayo yana urefu wa mita 35,232 yenye vipenyo mbalimbali .
Dk.Mbabaye amesema kuwa mabomba hayo yatagawiwa katika wilaya zote saba za Mkoa wa huo ambapo Kongwa mita 7,100,Bahi mita 600,Chemba mita 2,550 ,Mpwapwa mita 4,691,Kondoa mita 7,500,Chwamwino mita 5,581na Dodoma Jiji mita 7,210.
”Mpango huo utarejesha huduma ya maji katika vituo 2,059 visivyotoa huduma hiyo katika wilaya hizo na utawanufaisha wananchi 1,324,255 sawa na asilimia 61.9 ya wakazi 2,139,450 waishio maeneo ya Vijijini katika Mkoa wa Dodoma”amesema Dk.Mbabaye
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini ,Anthony Mavunde amesema kuwa kuna baadhi ya miradi iliyokuwa ikitekelezwa na Wizara ya Maji kupitia mradi wa DDCA haikufanya vizuri kutokana na kushindwa kukamilishwa kwenyei jimbo lake.
”Kuna miradi 13 ya maji ambayo inatekelezwa Jijijni hapo lakini kuna baadhi imekwama kutokana na kukwamishwa na rasilimali fedha ambazo zilikuwa zikitolewa na wahusika wa utekelezajiwa mradi”amesema Mavunde