Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zuena Omary akiongoza wafanyakazi wenzake kufanya zoezi maalum la kupambambana na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo Uvico-19.
Wafanyakazi wa sekta mbalimbali wa Mkoa wa Shinyanga wakifanya zoezi maalum la kupambambana na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo Uvico-19.
******************************
Na Anthony Ishengoma- Shinyanga
Wafanyakazi wa Sekta mbalimbali katika Mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Jasinta Mboneko wamefanya mazoezi ya kuimarisha kinga na kujiweka sawa dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo ugonjwa wa Uvico-19.
Wfanyakazi hao wamejitokeza kufanya mazoezi hayo yaliyofanyika katika uwanja wa CCM Kambarage na kuitikia wito wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati unaowataka wafanyakazi hao kufanya mazoezi kila siku kwa ajili ya kujikinga na Corona.
Akiongea mara baada ya kufanya mazoezi hayo Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Jasinta Mboneko alisema mazoezi ni Afya na tunavyoendelea na kupambana na ugonjwa huu wa Uviko- 19 ni lazima tufanye mazoezi lakini pia tuzingatie lishe bora vinginevyo hatuwezi kuwa na Afya Nzuri.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuena Omary amewambia watumishi hao kuwa tunafanya mazoezi haya uku kila mmoja wetu anafahamu kuwa kuna ugonjwa wa Uviko -19 hivyo mazoezi kama haya yanatuweka vizuri katika mwili wetu kwa kutufanya tuweze kupambana magonjwa ikiwemo magonjwa ya mshituko.
Bi. Zuena Omary ameongeza kuwa mazoezi haya yanatuweka pamoja kama ndugu na kutufanya tuishi pamoja na kufahamiana lakini pia kujenga afya ya mwili na akili kwa maendeleo yaetu kama familia ya moja ya wanamichezo.
Naye Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Jnawet Elias ameviambia vyombo vya habari kuwa mazoezi haya yanasaidia katika kupambana na corona na yatafanyika kila jumamosi na hakusita kutoa pongezi zake kwa Mkuu wa Mkoa kwa kuanzisha mazoezi hayo.
Wakati huohuo kiongozi wa mazoezi hayo Bw. Wiliam Masala kitendo cha Mkuu wa Mkoa kuanzisha mazoezi hayo kimnefanya wale waoga wa mazoezi kujitokeza kufanya hivyo kwa kujificha nyuma ya masa hiyo kupata tiba inayotokana na zoezi hilo.