*****************************
January 2021, Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. David Silinde alifanya ziara Mkoani Mtwara na kutembelea Shule ya Msingi Namalombe iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu na kukuta shule hiyo ikiwa na darasa 1 linalotumika na madarasa 2 yanayojengwa kwa nguvu za Wananchi yakiwa kwenye hatua ya Lenta na Choo kinachotumika na cha nyasi.
Jitihada za Makusudi zilifanyika kuhakikisha kuwa mazingira ya kufundisha na kujifunzia yanaboreshwa.
Naibu Waziri Silinde aliagiza Halmashauri ya Nanyama kukamilisha ujenzi wa madarasa hayo yaliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi kwa kutumia mapato ya Ndani na mpaka hivi sasa Halmashauri hiyo imekamilisha ujenzi wa madarasa hato katika shule ya msingi Namalombe.
Halkadhalika Ofisi ya Rais TAMISEMI ilipeleka Tsh. Mil 51 kwa ajili ya kuongeza madarasa nawili na matundu 10 ya vyoo na mpaka hivi dasa ujenzi unaendelea.
Sasa mazingira ni bora kabisa kwa Wanafunzi wa Namalombe kujifunza.
Hii ndio Kazi yetu Kuboresha Mazingira ya Kujifunza na kufundishia.
Namalombe sasa kama panavutia.