Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza na Viongozi wa Mabaraza ya Kidini na Mashirikisho ya Dini katika Kikao kilichofanyika jijini Dodoma leo. Amesema zoezi la mabadiliko ya hadhi ya Vyeti vya Usajili wa Jumuiya kutoka kuwa vya kudumu na kuwa vya kuhuishwa kila baada ya miaka 5 kwa sasa litahusisha Vyama vya Kijamii tu badala ya Taasisi za Kidini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Fredrick Shoo akizungumza katika kikao cha Viongozi wa Mabaraza ya Kidini na Mashirikisho ya Dini na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (hayupo pichani), jijini Dodoma, leo. Waziri alisema zoezi la mabadiliko ya hadhi ya Vyeti vya Usajili wa Jumuiya kutoka kuwa vya kudumu na kuwa vya kuhuishwa kila baada ya miaka 5 kwa sasa litahusisha Vyama vya Kijamii tu badala ya Taasisi za Kidini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza na Viongozi wa Mabaraza ya Kidini na Mashirikisho ya Dini katika Kikao kilichofanyika jijini Dodoma leo. Amesema zoezi la mabadiliko ya hadhi ya Vyeti vya Usajili wa Jumuiya kutoka kuwa vya kudumu na kuwa vya kuhuishwa kila baada ya miaka 5 kwa sasa litahusisha Vyama vya Kijamii tu badala ya Taasisi za Kidini. Picha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
…………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, MOHA.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema zoezi la mabadiliko ya hadhi ya Vyeti vya Usajili wa Jumuiya kutoka kuwa vya kudumu na kuwa vya kuhuishwa kila baada ya miaka 5 kwa sasa litahusisha Vyama vya Kijamii tu badala ya Taasisi za Kidini.
Awali, Zoezi hili ambalo limeanza Agosti 16, 2021 lililenga kuhusisha Taasisi za Kidini na Jumuiya za Kijamii, lakini kwa sasa zoezi hili litahusisha Vyama vya Kijamii pekee hadi hapo Serikali itakapoamua Vinginevyo.
Waziri Simbachawene ameyasema hayo katika Kikao chake na Viongozi wa Mabaraza ya Kidini na Mashirikisho ya Dini mbalimbali Nchini kilichoketi jijini Dodoma leo.
“Tumeona kuwa ni vyema kwa sasa zoezi hili likahusisha Jumuiya za Kijamii 8,851 tu na halitahusisha Taasisi za Kidini, hadi pale Serikali itakapoamua vinginevyo”. Alisema Simbachawene.
Uamuzi wa Kutohusisha Taasisi za Kidini, umekuja baada ya Kikao baina Waziri wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi na Viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kidini kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijijni Dodoma.
Waziri Simbachawene aliongeza kuwa, jumla ya Vyama vya Kijamii 8,851 ndizo zitakazohusishwa katika zoezi linaloendelea hivi sasa, kupitia Ofisi ya Msajili wa Jumuiya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kwa upande wake Msajili wa Jumuiya, Emmanuel Kihampa alisema kufuatia mabadiliko hayo, Vyama vyote vya Kijamii nchini Vinaagizwa kufika katika Ofisi ya Msajili wa Jumuiya iliyopo Ghorofa ya 11 katika Jengo la Kambarage Jijini Dodoma, kwa lengo la kuhuisha usajili wake na kupatiwa vyeti vipya vya usajili.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Wailsam Tanzania (BAKWATA), Shekhe Hamis Mataka alimshiukuru Waziri pamoja na uongozi wa Wizara kwa kukutana na viongozi wa dini katika mkutano huo.
“Leo tunafuraha, Waziri upo, Naibu Waziri, Katibu Mkuu pamoja na Msajili wetu, hii inatusaidia hata migogoro mbalimbali yakidini inayokusumbua mheshimiwa Waziri kwa kukutana huku kunakusaidia endapo itatengenezewa njia kupitia kukutana katika umoja huu,” alisema Shekhe Mtaka.
Mwisho/-