****************************
Agost 16
Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga
KIONGOZI wa mbio maalum za mwenge wa Uhuru ,LT.Josephine Mwambashi ameeleza ni wajibu kuisaidia Serikali, kuzuia na kupambana na matumizi ya madawa ya kulevya na kuwafichua wanaozalisha dawa za kulevya na wafanyabiashara wakubwa wa madawa hayo .
Ameeleza, jamii inapaswa kusaidia vyombo vya dola hususan polisi kuwabaini wakulima wa bangi na wauzaji pamoja na wasafirishaji .
Akitembelea mradi wa mapambano dhidi ya dawa za kulevya, Kilimahewa ,Mwambashi alielezea ,dawa za kulevya zina punguza nguvu kazi na kuhatarisha afya ya watumiaji ambao hupata athari za kiakili na kupata magonjwa yatokanayo na zinaa .
“Ni jukumu letu kuisaidia Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu, kupambana na matumizi hayo,wanaozalisha dawa ya kulevya kwasababu dawa ya kulevya kama mirungi,bangi zinazalishwa nchini kwetu na baadhi ya wakulima wanatumia nafasi hizo kuzalisha mazao mchanganyiko na bangi”
Nae mkuu wa wilaya ya Mkuranga ,Hadija Nasir Ally alieleza ,amepokea mwenge wa Uhuru ,agost 16 ukitokea wilaya ya Kibiti,ambapo ukiwa Mkuranga mwenge huo utatembelea miradi 15 yenye thamani ya sh bilioni 21.1.
Kuhusiana na mapambano dhidi ya dawa za kulevya ya wilaya , taarifa ilieleza vijana 34 wanahudumiwa katika vituo vya kutolea huduma za afya .
Inasema wilaya hiyo ,imefanikiwa kutoa elimu kufanya utambuzi wa waathirika wa dawa za kulevya na kuwashawishi kuanzisha vikundi vya ujasiriamali ili kujipatia kipato .
Muathirika wa madawa ya kulevya Kudra Ibrahim alisema wapo wanne ,ambao wameamua kutumia methadon kuachana na madawa ya kulevya na kujidunga.
Mwenge huo ukiwa Mkuranga,pia umetembelea mradi wa uwezeshaji wa wanawake kiuchumi ,kikundi cha wanawake cha wanawake cha Muungano Kilimahewa Kaskazini chenye wanachama tisa, na wanafuga kuku wa asili.
Pamoja na miradi hiyo, kuna mradi uliozinduliwa wa skimu ya maji Mkerezange ,Mkamba ambapo unatarajia kuhudumia Kijiji cha Kigoda na Mkerezange vyenye wakazi 2,550.