Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul kushoto akisitiza jambo kwa wanamichezo walioshiriki mashindano ya Olimpiki 2020 na wanaotarajia kushiriki mashindano hayo kwa watu wenye ulemavu (Paraolyimpic) hawapo pichani Wakati alipowapokea na kuwaaga wachezaji hao iliyofanyika jana 12 Agosti 2021 jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Michezo toka Wizara hiyo Yusuph Singo na kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo (BMT), Neema Msitta.
Mkurugenzi wa Idara ya Michezo toka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yusuph Singo(kulia) akizungumza na wanamichezo walioshiriki mashindano ya Olimpiki 2020 na wanaotarajia kushiriki mashindano hayo kwa watu wenye ulemavu (Paraolyimpic) hawapo pichani Wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wachezaji hao jana 12 Agosti 2021 jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo (BMT), Neema Msitta (kulia) akizungumza na wanamichezo walioshiriki mashindano ya Olimpiki 2020 na wanaotarajia kushiriki mashindano hayo kwa watu wenye ulemavu (Paraolyimpic) hawapo pichani Wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wachezaji hao iliyofanyika jana 12 Agosti 2021 jijini Dar es Salaam.
Wanamichezo walioshiriki Mashindano ya Olimpiki 2020 nchini Japan wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (hayupo pichani) Wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wachezaji hao iliyofanyika jana 12 Agosti 2021 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa vyama vya michezo wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (hayupo pichani) Wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wanamichezo walioshiriki mashindano ya Olimpiki 2020 na wanaotarajia kushiriki mashindano hayo kwa watu wenye ulemavu (Paraolyimpic) iliyofanyika jana 12 Agosti 2021 jijini Dar es Salaam.
Kiongozi wa msafara wa wanamichezo walioshiriki mashindano ya Olimpiki 2020 Henry Tandau akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (hayupo pichani) Wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wanamichezo walioshiriki mashindano ya Olimpiki 2020 na wanaotarajia kushiriki mashindano hayo kwa watu wenye ulemavu (Paraolyimpic) iliyofanyika jana 12 Agosti 2021 jijini Dar es Salaam.
Mwanariadha aliyeshiriki mashindano ya Olimpiki 2020 nchini JapanAlphonce Simbu akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (hayupo pichani) Wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wanamichezo walioshiriki mashindano ya Olimpiki 2020 na wanaotarajia kushiriki mashindano hayo kwa watu wenye ulemavu (Paraolyimpic) iliyofanyika jana 12 Agosti 2021 jijini Dar es Salaam.
rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Gulam Rashid (kushoto) akizunumza Wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wanamichezo walioshiriki mashindano ya Olimpiki 2020 na wanaotarajia kushiriki mashindano hayo kwa watu wenye ulemavu (Paraolyimpic) iliyofanyika jana 12 Agosti 2021 jijini Dar es Salaam, katikati ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Michezo toka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yusuph Singo.
Mwanariadha aliyeshiriki mashindano ya Olimpiki 2020 nchini Japan Alphonce Simbu (kushoto) akimkabidhi bendera ya Taifa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul Wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wanamichezo walioshiriki mashindano ya Olimpiki 2020 na wanaotarajia kushiriki mashindano hayo kwa watu wenye ulemavu (Paraolyimpic) iliyofanyika jana 12 Agosti 2021 jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (kulia) akimkabidhi tiketi za ndege mshiri wa mashinda ya Olimpiki kwa watu wenye ulemavu (Paralimpiki) Bi. Sauda Njopeka Wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wanamichezo walioshiriki mashindano ya Olimpiki 2020 na wanaotarajia kushiriki mashindano hayo kwa watu wenye ulemavu (Paraolyimpic) iliyofanyika jana 12 Agosti 2021 jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (kushoto) akiwakabidhi bendera ya Taifa washiriki wa mashindano yaOlimpiki kwa watu wenye ulemavu Wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wanamichezo walioshiriki mashindano ya Olimpiki 2020 na wanaotarajia kushiriki mashindano hayo kwa watu wenye ulemavu (Paraolyimpic) iliyofanyika jana 12 Agosti 2021 jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanamichezo walioshiri mashindano ya Olimpiki 2020 nchini Japan Wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wanamichezo hao iliyofanyika jana 12 Agosti 2021 jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul (wa pili toka kushoto waliosimama ) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanamichezo watakaoshiriki mashindano ya Olimpiki 2020 kwa watu wenye ulemavu nchini Japan Wakati wa hafla fupi iliyofanyika jana 12 Agosti 2021 jijini Dar es Salaam.
****************************
Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Pauline Gekul (Mb) amewataka watanzania kutopuuzia Jitihada zilizoonyeshwa na wachezaji wa Timu ya Taifa ya Riadha waliokwenda kushindana katika mashindano ya Olimpiki 2020 nchini Japan na kufanikiwa kuingia katika nafasi ya kumi (10) bora kwenye mbio ndefu za kilomita 42 Barabarani.
Mhe. Pauline ameyasema hayo tarehe 12 Agosti, 2021 wakati akiipongeza Timu iliyoshiriki katika mashindano ya Olimpiki na kuiaga Timu inayokwenda kushiriki mashindano ya Paralimpiki nchini Japan, katika hafla iliyofanyika katika hotel ya Blue Sapphire Jijini Dar es Salaam.
“niombe watanzania wasipuuze jitihada zilizofanywa na wachezaji wetu wa riadha katika mashindano ya Olimpiki, bali tunatakiwa kuwapongeza kwa kulipambania Taifa katika mashindano hayo makubwa duniani licha ya kuwa na mabadiliko ya hali ya hewa lakini walipambana na tukamaliza katika nafasi ya kumi bora kwa mwanariadha wetu Alphonce Simbu kushika nafasi ya saba,tunatakiwa tujifunze kuthamini wa kwetu,”amesema Pauline.
Aidha Mhe. Pauline amesema wizara yenye dhamana ya michezo inayosimamiwa na Mheshimiwa Waziri Innocent Bashungwa imedhamiria kuendelea kuinua michezo nchini pamoja na kuipa nguvu michezo ya kipaumbele iendelee kufanya vizuri.
“ndugu zangu naomba ifahamike kuwa wizara yetu inayoongozwa na Mhe. Bashungwa imedhamiria kuendelea kuinua michezo nchini, lakini pia michezo ya kupaumbele tutaendelea kuipa nguvu iendelee kufanya vizuri,niseme tu kwamba viongozi wa vyama ambao hawawajibiki wajitathmini, Serikali yetu ya awamu ya Sita (6) inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ipo makini na haitawafumbia macho viongozi wa michezo ambao hawawajibiki,”amesema Mhe. Pauline.