Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu akikagua ujenzi wa Kituo cha afya cha Makowo, Halmashauri ya Mji Njombe na kusisitiza umuhimu wa wakurugenzi kuhakikisha wanatenga fedha za mapato ya ndani kutatua kero za wananchi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na wananchi wa kijiji cha Makowo , kata ya Makowo, Halmashauri ya Mji Njombe mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye Kituo cha afya cha Makowo.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Makowo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu alipotembelea kituo cha Afya Makowo, Halmashauri ya Mji wa Njombe
Waziri wa Ncho Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na wananchi wa kijiji cha Makowo , kata ya Makowo, Halmashauri ya Mji Njombe mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye Kituo cha afya cha Makowo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhandisi Marwa Mwita Rubirya alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika kituo cha afya cha Makowo, Halmashauri ya Mji Njombe.
***************************
Na. Angela Msimbira NJOMBE
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu amesema kuwa yeye ni waziri wa vijijini kwa kuwa ndipo wananchi wanyonge walipo na ndipo kero za wananchi zilipo zikiwemo kero za barabara, Maji, Elimu na afya.
Akiongea na wananchi wa kijiji cha Makowo katika kata ya Makowo, Mkoani Njombe leo wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa Kituo cha afya cha Makowo Waziri Ummy amesema atatembelea maeneo ambayo hayafikiki kwa lengo la kutatua changamoto zao hasa kwenye maneneo ya vijijini ambapo ni mbali kufikika.
“Maeneo ya pembezoni mwa miji hasa vijijini ndipo kwenye shida nyingi ambazo zinahitaji kutatuliwa, Nikiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi nimebeba dhamana kubwa ya kutatua kero hizo na kuzitatua kwa wakati lengo ni kuwasaidia wananchi wanyonge na kuleta maendeleo kwa jamii.” Amesema Waziri Ummy.
Akijibu kero za wananhi wa Kata ya Makowo Waziri Ummy alitumia nafasi hiyo kuwapongeza wananchi hao kwa kuibua mradi wa ujenzi wa Kituo cha afya Makowo kwa kutumia nguvukazi na mali katika ujenzi wa kituo hicho kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhakikisha wanachangia katika kuleta maendeleo ,hivyo aliahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya ununuzu wa vifaa na vifaa tiba na gari la wagonjwa ili kituo hicho kianze kutoa huduma kwa wananchi na kupunguza vifo vya wamama wajawazito wanaotembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Aidha, aliwapongeza Halmashauri yaMji wa Njombe kwa kutumia fdha za mapato ya ndani kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho na kusema kuwa amefurahishwa kwa Halmashauri hiyo kutumia mapato hayo kutatua kero za wananchi na sio kutumika kwa ajili ya semina na makongamano.
Amesema kuwa Fedha za Mapato ya Ndani kazi yake kubwa ni kutatua kero za wananchi, hivyo amewaagiza Wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kutatua kero za wanannchi na miradi ya kimakakati ambayo inaleta tija kwa jamii.
Kwa upande wa ujenzi wa miundombinu ya barabara Waziri Ummy amesem Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani amejikita katika kuimarisha barabara za mijini na vijijini ambapo katika bajeti ya ujenzi wa miundombinu ya barabara imeongezeka kutoka shilingi bilioni 8 kwa mwaka 2020/2021 hadi kufikioa shilingi bilioni 19 kwa mwaka 2021/2022.
Amefafanua kuwa kwa upande Halmashauri ya Mji wa Njombe kwa mwaka wa fedha 2020/2021 haikuwa imepangiwa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya barabara lakini katika mwaka wa fedha 2021/2022 serikali imetenga kiasi cha shilingi biloni 4.3 lengo likiwa ni kuhakikisha barabara za vijijini zinafunguliwa.
Vilevile Waziri Ummy amesema Serikali itatoa kiasi cha shilingi cha shiliningi bilioni 120 kwa ajili ya ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha changarawe katika eneo la kijiji cha Makowa ili iweze kupitika wakati wote lengo ni kubadilisha maisha ya wananchi wa vijijini.
Kwa upande wa elimu Waziri Ummy amesema kuwa serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni 12.5 boma moja kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma hivyo amewaagiza wananchi kujiongeza kwa kuchangia maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya Serikali ili kuunga mikono Serikali.
Waziri Ummy yupo kwenye ziara ya kikazi katika Mkoa wa Njombe ambapo leo amekagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Mji wa Njombe kwa kuweka jiwe la msingi katika Kituo cha afya Makowo, kuzindua ujenzi wa Madarasa ya shule ya sekondari ya Matola na kukagua ujenzi wa barabara ya utalingolo