Kaimu Msajili wa Bodi ya Wathamini Joseph Shewiyo akitoa maelezo ya awali leo wa wakati wa ufungaji wa mafunzo ya wathamini siku 12 yalifanyika mjini Tabora
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo akifunga jana mjini Tabora ya mafunzo ya siku 12 kwa Wathamini mali 72 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini.
Baadhi ya Wathamini mali 72 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku 12 yalifanyika mjini Tabora.
Mtathimini kutoka Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali Baraka Molleli akitoa maelezo jana mjini Tabora kwa niaba ya wenzake wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku 12 yalifanyika mjini Tabora.
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa salamu za Mkoa jana wakati wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku 12 yalifanyika mjini Tabora
Picha na Tiganya Vincent
******************************
NA TIGANYA VINCENT
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo amewataka Wathamini mali kutogeuza Ofisi sehemu kuwashawishi kupata fedha kutoka kwa wananchi wanyonge.
Alisema vitendo vya aina hiyo vinaacha mauvimu kwa wananchi wanyonge na kufanya walie machozi ya uchungu baada ya kupewa thamani ndogo ya mali zao na kulipwa fidia kidogo ya kiasi anachotakiwa kupata.
Alisema baadhi ya Wathamini wasio waaminifu wamekuwa wakifanya tathimini ya mali za wananchi wanyonge kwa kiwango cha chini kwa ajili ya kuwakandamizakwa lengo kutaka kuwashiwishi wawepe rushwa.
Mary aliongoza kuwa wapo baadhi yao wamekuwa wakitathimini kwa kuongeza na wengine kupunguza thamani ya mali tofauti na hali halisi kwa maslahi binafsi na kuisababishia Serikali hasara kubwa.
Alisema wapo baadhi ya Wathamini wanashirikiana na watumishi wa Taasisi za fedha kufanya tathimini mali hewa ikiwemo kuonyesha uwepo wa nyumba wakati haipo na kusababisha hasara kwa Taasisi hizo.
Mary alisema kuwa baadhi yao wamekuwa wakichelewesha kwa makusudi kazi za uthamini bila sababu kwa lengo kuweka mazingira ya kushawishi kupewa rushwa.
Katibu Mkuu huyo aliitaka Bodi ya Wathamini kuwachukulia hatua za kinidhamu ikiwemo kuwanyang’anya leseni za ufanyakazi Wathamini ambao watabainika kukiuka maadili ambao utafanya taalumu hiyo kushuka hadhi katika jamii.
Aidha Mary aliwataka wahitimu hao wa Utathimini kufungua ukurasa upya na kufanya jamii kuwaamini kwa kutenda kazi zao kwa uadilifu na uzalendo zaidi.
Mtathimini kutoka Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali Baraka Molleli alisema kuswa baada ya mafunzo hayo watakwenda kuwa kioo kwa wafanyakazi wenzake.