……………………………………………………………………..
Wazee wa Mji wa Mafinga wameipongeza Serikali kwa kuweka utaratibu wa kuwepo Dirisha Maalum la kuwahudumia Wazee lakini wakatoa angalizo kuwa utaratibu huo usiwe kwa maandishi Bali kwa vitendo.
Wakizungunza wakati wa Mkutano wa ndani wa Wazee na Viongozi wa Dini wa Mji wa Mafinga ulioitishwa na Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi kwenye Ukumbi wa CCM, Wazee Hao Wamesema kuwa Mara nyingi wanakaa foleni katika kupata huduma licha ya kuwepo kwa maandishi yasemayo Mpishe Mzee Ahudumiwe
Utaratibu wa kuwepo kwa dirisha maalum la kuwahudumia Wazee ni mzuri lakini Mara nyingi hatutendewi kama tunavyostahili, alisema Mzee Msuva.
Akifafanua hoja hiyo, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga Dkt Innocent Mhagama alisema kuwa wanatamani sana kuwahudumia Wazee kwa wakati lakini uhaba wa watumishi Umekuwa kikwazo katika kutoa huduma kwa Wazee kwa ufanisi.
Katika kukabiliana na changamoto hii tumeelezana kuwa ukimuona Mzee kwenye foleni mchukue apate huduma kwanza, lakini tunatoa wito kwa jamii kuwapisha Wazee wapate huduma kwanza, alisisitiza Dkt Mhagama.
Mapema akiwasalimia Wazee na Viongozi wa Dini, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Saad Mtambule amesema kuwa ni dhamira yake kuhakikisha kuwa anawatumia Wazee na Viongozi wa dini katika kushughulikia kero za wananchi na hasa migogoro ya Ardhi.
Akitoa neno la Shukran, Mzee Ngogo alimpongeza mbunge wa Jimbo hilo Chumi kwa kuweka utaratibu wa kukutana na Wazee na Viongozi wa dini.
Katika salaam zake kwa Wazee na Viongozi wa dini,Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndugu Yasin Daud aliwapongeza Wazee kwa kuitika wito wa mbunge wao na kuwaomba kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi wa Viongozi wa Baraza la Wazee wa Wilaya ya Mufindi.
kwa utaratibu huu, sisi Wazee tunafarijika kuwa unatuheshimu, nasi tutakuwa wepesi kukushauri, Wazee hawataki mambo mengi, Isipokuwa kuheshimiwa aliisema Mzee Ngogo.