Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Joseph Mkirikiti (pichani) akiongoza zoezi la kupata chanjo ya kinga dhidi ya virusi vya Corona leo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga ambapo uzinduzi rasmi ulifanyika. 

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Rainer Lukala akipata chanjo ya UVIKO-19  leo mjini Sumbawanga  wakati wa uzinduzi rasmi kwenye mkoa huo.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface Kasululu  akipata chanjo ya kinga dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona leo kwenye uzinduzi uliofanyika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga. 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Dunstan Ndunguru akipata chanjo ya UVIKO-19  leo mjini Sumbawanga  wakati wa uzinduzi  .

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Rashid Akilimali akipata chanjo ya kinga dhidi ya UVIKO-19  leo mjini Sumbawanga 

ehemu ya wananchi wa Mkoa wa Rukwa waliojitokeza leo kwenye uzinduzi wa zoezi la utoaji chanjo ya kinga dhidi ya UVIKO-19 leo kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga. 
 
( Habari na Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
*******************************

Wananchi wa mkoa wa Rukwa wamehamasishwa kjitokeza kupata chanjo ya kinga dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona ambapo serikali mkoa wa Rukwa imeanza kutoa chanjo kwa wananchi wenye utayari na hiari .

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Joseph Mkirikiti  leo (04.08.2021) amewaongoza wananchi wa mkoa huo kupata chanjo ya kinga dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona ambapo amesema kuwa chanjomhiyo ni salama na inalenga kuwasaidia watu kuwa na kinga imara .

Mkuu huyo amewaeleza wakazi wa Sumbawanga waliokusanyika kwenye hospitali  ya Rufaa ya Mkoa Sumbawanga kuwa serikali ya Awamu  ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imedhibitisha pasipo shaka kuwa chanjo hii ya UVIKO  19 ni salama na kuwa wengi wajitokeze kupata chanjo.

“Rais Samia amesema chanjo hii ni bure na ya hiari kwa mwananchi yeyote mwenye kuhitajinili kujikinga na ugonjwa wa Corona. Mimi leo nitakuwa wa kwanza kuchanja hapa hapa ” alisema Mkirikiti

Katika tukio hilo lililohudhuriwa na viongozi wa serikali na dini , wazee maarufu pamoja na wananchi toka wilaya zote za Sumbawanga, Nkasi na Kalambo  wananchi  wengi wamehamasika kupata chanjo hiyo.

Mkirikiti  ameto agizo kwa wakuu wa wikaya kutoa elimu kwa kushirikiana na viongozi wa dini juu ya kudhibiti mikusanyiko na kwenye shughuki za misiba ili kuepuka maambukizi kusambaa.

Mkuu huyo wa mkoa alisisitiza wataalam wa afya kutoa elimu ya kujikinga ikiwemo umuhimu wa kufanya mazoezi hatua itakayosaidia kuongeza kinga ya mwili dhidi ya virusi vya Corona.

Akizungumza kuhusu chanjo hiyo Mganga Mkuuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface Kasululu  alisema lengo la serikali  kutoa dozi hizo za chanjo ya kinga dhidi ya ugonjwa wa virusi  vya Corona utasaidia kuongeza kinga ya mwili ya mwanadamu .

Aliongeza kusema lengo jingine ni kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa pia kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na virusi vya Corona.

” Tumepokea dozi za chanjo Elfu Ishirini ambazo tayari zimefikishwa kwenye vituo 11 vilivyoanishwa kutoa chanjo, wananchi naomba tujitokeze kupata chanjo” alisema Dkt. Kasululu

Naye Mzee maarufu wa Sumbawanga Kapteni Mstaafu Nkoswe Noel (81) amefurahi kupata chanjo hiyo na kuiomba serikali kuwafikishia wananchi wengi chanjo ili waepukane na ugonjwa huu hatari wa korona.

Mzee Nkoswe amewasihi wakazi wa Rukwa kujitokeza na kuchanja ili maradhi ya Corona  yasiendelee kuenea nchini  na kuongeza kuwa serikali ilete chanjo zaidi ya 20,000 za sasa.

Kwa upande wake Sheikh wa Mkoa wa Rukwa Rashid Akilimani akizungumza  baada ya kupata chanjo ya UVIKO 19 alisema ameshukuru kupata dozi hiyo kwani itamwezesha mwaka huu kwenda kutekeleza ibada ya Hija.

” Mwaka jana 2020 sikuweza kwenda Hija nchini Saudia baada ya kukosa chanjo ya UVIKO. Leo ninashukuru serikali kutuletea chanjo hii hapa Rukwa” alisema Sheikh Akilimali.