Mwanachama wa chama cha Tanganyika Afrikani National Union (TANU ) mzee Omary Nzowa mkazi wa mkoa wa Iringa akionyesha picha ya wanachama wa TANU mkoa wa Iringa ambao wengi wao wamekwisha fariki dunia ,jana wakati akizungumza na wanahabari (picha na Francis Godwin.
***************
NA FRANCIS GODWIN, IRINGA
Mwanachama wa chama cha Tanganyika Afrikani National Union (TANU ) mzee Omary Nzowa mkazi wa mkoa wa Iringa amewataka vijana nchini kuwa wazalendo na Taifa kama ilivyokuwa kwa vijana wa enzi za TANU ambao hawakutanguliza maslahi yao mbele katika kulitumikia Taifa .
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana ofisini kwake Nzowa alisema kuwa wakati wa chama cha TANU vijana na wachama wote walijitolea mali zao kwa ajili ya chama na chama hicho kilikuwa na heshima kubwa na hata kama dini zingechelewa kufika basi watanzania wote dini yao ingekuwa na TANU tofauti na sasa watu kutanguliza maslahi mbele badala ya uzalendo.
“ Heshima kubwa iliyokuwepo kwa wanachama wa TANU na imani kubwa walioonyesha kwa chama hicho na uzalendo waliokuwa nao TANU ingekuwa ni dini ya watanzania kama dini zilizopo sasa zisingeingia nchini nataka kusema kuwa mwanachama wa TANU ukitembea na kadi yako ulikuwa unaheshimika na hata ukisafiri kwenye basi kama huna nauli ukionyesha kadi abiria wanakuchangia nauli yako “alisema
Kwa sasa hali hiyo ya uzalendo na kuheshimiana inazidi kushuka kwani watu wametanguliza mbele maslahi yao badala ya uzalendo na ujamaa .
“ Ukiniambia nielezee ugomvi uliopo sasa na hali iliyopo sasa nchini ni ugomvi wa maslahi lakini wato walijitolea mali zao walijitolea nyumba zao kwa ajili ya chama cha TANU na hakukuwa na malipo yoyote kuanzia katibu hadi chini ilikuwa ni bure kujitolea “ alisema Nzowa
Kuwa kwa sasa ni wakati tofauti sana na dunia imebadilika kwa chama kuwa maslahi hivyo kuna haja kubwa sana ya kueneza umoja wa watanzania hasa ukizingatia sasa kizazi kilichoanzisha TANU si kizazi kilichopo sasa kwani kizazi kile cha TANU kilikuwa na utayari kwa sababu wameuona utawala wageni wakoloni ndio maana walikuwa na mshikamano .
Nzowa alisema kuwa maombi yake kwa watanzani kuonyesha mshikamano wa kizalendo kwa sasa kwa sababu hata vijana wengi wametembea na kuona na hata ukiwauliza leo utawasikia wakisema kuwa Marekani na Uingereza hawafanya kama sisi wanataka Taifa kuendelea kutawaliwa kwa kuwa kutawaliwa si bendera bali hata mawazo ya kutoipenda nchi yako ni wazi kwa vijana wenye mawazo hayo ni wale wasio na uzalendo .
“ Ushauri wangu kwa vijana ambao wanapenda kutolea mifano ya mataifa mengine badala ya kutanguliza uzalendo kujaribu kuwatafuta wazee walioopata kuona utawala uliopita na kufuatilia maisha ya wanachama wa TANU jinsi walivyoishi kizalendo na kudumu na mawazo hayo kama njia ya kulifanya Taifa la kizalendo “
Nzowa akizungumza huku akionyesha picha iliyopigwa enzi za TANU na wanachama wa TANU mkoa wa Iringa alisema katika picha hiyo yenye zaidi ya watu 10 wanachama wa TANU ni mwanachama mmoja pekee ambae ni hai na kuwa mwanachama huyo alipata kuwa mkuu wa wilaya na mkuu wa mikoa mbali mbali ila wapo wanachama kama mzee Mohamed Amer Abri ukiangalia sasa kupitia kizazi hicho kuna wajukuu zake akina Salim Abri ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) mkoa wa Iringa na Arif Abri ni mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa .
Kuwa misingi ya bora ya uzalendo kwa familia ambazo zimetokana na TANU ambazo ni chache imeendelea kulifanya Taifa kuwa imara japo kuna haja uzalendo huo kuenezwa zaidi kama njia ya kulifanya Taifa kuishi kama enzi za TANU.
“ Ushahidi wa picha hii na eneo ilipopigiwa ndipo ilikuwa ofisi ya TANU Iringa na huyu mzee Mohamed Abri ni mzee ambae alijichanganya na wananchi na familia nzima ilikuwa imejichanganya na wananchi na kwenda pamoja katika kutafuta uhuru wa nchi yetu na nyumba hii iliyoanzia TANU mwenyenyumba alikuwa akiitwa Omray Albart ambae amekwisha kufa ila baada ya chama kuondoa ofisi hapo nyumba hiyo iliuzwa ila ushauri wangu kwa vijana uzalendo nin itikadi na ukiwa mzalendo utapenda kujua historia ya akina nani ambao walipingania nchi kufika hapa “ alisema Nzowa
Kuwa kama vijana watatanguliza uzalendo badala ya maslahi nchi hii itazidi kuheshimika daima na wazee wataendelea kuheshimika kwani nchi ilipofikia kwa sasa wapo watu ambao waliifanya iwe hivi sasa kwani walipoteza mali zao na utu wao kwa ajili ya kuona nchi imepata uhuru .
“ Uhuru huu umepatikana kwa uvumilivu mkubwa na watu kujitolea na uhuru haukupatikana kwa urahisi ila ulipatikana kwa watu kujitolea na kipimo cha juu ni kuwa mzalendo na Taifa kuwa vijana wengi wanatanguliza maslahi ila kama wanachama wa TANU nao wangetanguliza maslahi nchi hii isingekuwa hapa ilipo leo .