Timu ya Azam FC kutoka Chamazi wametangaza rasmi kuachana na wachezaji wake wanne wa kimataifa wachezaji hao ni wasahambuliaji wawili ,Obrey Chirwa, Mpiana Monzinzi, Kiungo Mkabaji Ally Niyonzima pamoja na benki wao Yakubu Mohammed kwa makubaliano ya pande zote mbili .
Taarifa iliyotolewa na Klabu hiyo inasema kuwa ” Tumefikia makubaliano ya pande mbili ya kuachana na wachezaji wetu wanne wa kimataifa’ Wachezaji hao ni beki wa kati, Yakubu Mohammed, kiungo Ally Niyonzima, mshambuliaji Mpiana Monzinzi na Obrey Chirwa, ambaye mkataba wake umemalizika”
“Azam FC tunawashukuru kwa mchango wao waliotoa katika klabu hii bora kipindi chote walichokuwa nasi na tunawatakia kila la kheri huko waendako”
Baada ya kufunguliwa Dirisha la Usijali na Uhamsiho wa Kimataifa kwa Klabu za Tanzania kuanzia Julai 19, 2021 hadi Agosti 31, 2021,tayari Matajiri hao wa Chamazi,wameshasajili wachezaji watano ,wanne ni kutoka nje na mmoja akiwa mchezaji wa ndani.
Wachezaji hao ni mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Rodgers Kola, akitokea Zanaco, Kiungo mshambuliaji Charles Zulu kutoka Zambia alikuwa anacheza Cape Town City ya Afrika ya Kusini.
Wengine ni kiungo mshambuliaji wa Kenya, Kenneth Muguna akitokea Gor Mahia,kiungo mkabaji wa Zambia, Paul Katema, aliyetokea Red Arrows ya Zambia pamoja na beki wa Tanzania Edward Manyama akitokea Ruvu Shooting.
Azam FC msimu ujao watashiriki Mashindano ya Kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) baada ya kushika nafasi ya tatu katika Msimamo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (VPL).