Waziri wa Kilimo.Prof.Adolf Mkenda,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampuni Mpya ya PASS Leasing yenye lengo la kukopesha wakulima, wavuvi na wafugaji zana za kilimo bila dhamana yoyote hafla iliyofanyika wakati wa Wiki ya PASS Trust katika kwenye viwanja vya Nyerere Square, jijini Dodoma Julai 24,2021.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PASS Trust, Dkt. Tausi Kida,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampuni Mpya ya PASS Leasing yenye lengo la kukopesha wakulima, wavuvi na wafugaji zana za kilimo bila dhamana yoyote hafla iliyofanyika wakati wa Wiki ya PASS Trust katika kwenye viwanja vya Nyerere Square, jijini Dodoma Julai 24,2021.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Athony Mtaka,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampuni Mpya ya PASS Leasing yenye lengo la kukopesha wakulima, wavuvi na wafugaji zana za kilimo bila dhamana yoyote hafla iliyofanyika wakati wa Wiki ya PASS Trust katika kwenye viwanja vya Nyerere Square, jijini Dodoma Julai 24,2021.
Waziri wa Kilimo.Prof.Adolf Mkenda (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kampuni Mpya ya PASS Leasing yenye lengo la kukopesha wakulima, wavuvi na wafugaji zana za kilimo bila dhamana yoyote hafla iliyofanyika wakati wa Wiki ya PASS Trust katika kwenye viwanja vya Nyerere Square, jijini Dodoma Julai 24,2021.
Waziri wa Kilimo Prof.Adolf Mkenda (kulia), akimkabidhi ufunguo Anthony Maganga mara baada ya kumkabidhi trekta aina ya New Holland yenye thamani ya sh. nil. 54 ikiwa ni mkopo uliotolewa na Kampuni ya Mpya ya PASS Leasing. Anayeshuhudia katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PASS Trust, Dkt. Tausi Kida.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka (kulia), akimkabidhi namba Anthony Maganga mara baada ya kumkabidhi trekta aina ya New Holland yenye thamani ya sh. nil. 54 mkopo uliotolewa na Kampuni ya PASS Leasing.
Waziri wa Kilimo Prof.Adolf Mkenda, akimkabidhi ufunguo Lillian Maricky wa Kampuni ya Magic LN Suppliers ya Chalinze, mkoani Pwani ikiwa ni ishara ya kumkabidhi mitambo ya kuvuna mpunga yenye thamani ya sh. mil.79 mkopo uliotolewa na Kampuni ya PASS Leasing. Anayeshuhudia katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PASS Trust, Dkt. Tausi Kida.
Waziri wa Kilimo Prof.Adolf Mkenda (kulia), akimkabidhi ufunguo Gebe Millinga ikiwa ni ishara ya kumkabidhi trekta aina ya John Deere pamoja na majembe yake lenye thamani ya sh. mil. 71.4 mkopo uliotolewa na Kampuni ya PASS Leasing. Anayeshuhudia katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PASS Trust, Dkt. Tausi Kida. Gebe amepokea trekta hilo kwa niaba ya kaka yake Mwanzo Millinga anayefanya kazi ya kilimo mkoani Ruvuma.
Waziri wa Kilimo Prof.Adolf Mkenda akimkabidhi ufunguo Dickson Tesha ikiwa ni ishara ya kumkabidhi trekta aina ya New Holland lenye thamani ya sh. mil. 46 mkopo uliotolewa na Kampuni ya PASS Leasing. Tesha amepokea trekta hilo kwa niaba ya Japhet Ndebesi wa Chamwino, mkoani Dodoma.
…………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Kilimo Prof.Adolf Mkenda amezindua kampuni mpya ya PASS Leasing Company LTD inayomilikiwa na Taasisi ya PASS Trust yenye lengo la kutoa mikopo ya zana za kilimo bila dhamana yoyote.
Akizungumza leo Julai 24,2021 jijini Dodoma wakati akizindua kampuni hiyo pamoja na ufungaji wa wiki ya Taasisi ya PASS Trust (Private,Agriculture Sector Support Trust)iliyoandaliwa na Taasisi hiyo kuanzia Julai 21 hadi Julai 24 kwa lengo la kuchagiza masuala ya kilimo nchini.
Prof.Mkenda amesema kuwa lengo ya wiki ya PASS ilikuwa ni kuwakutanisha wakulima,wauza zana za kilimo,taasisi za kifedha,wauza pembejeo,viongozi wa Serikali na wachakataji katika kuzungumzia maswala ya upatikanaji wa fedha kama kichocheo cha ukuaji wa kilimo biashara.
“PASS imekuwa itoa dhamana ya mikopo kuanzia asilimia 20 -60( hadi asilimia 80 kwa wanawake) kwa benki shiriki kama njia ya kuongeza dhamana ya kutosha ili kuwezesha wateja kupata mikopo,”amesema
Hata hivyo ameipongeza PASS kwa kuandaa wiki hiyo kwa kuwakutanisha wadau mbalimbali na kuwataka kwenda kujifunza zaidi na kuwa bora kutokana na kongamani hilo
Aidha amesema kuwa Serikali inatarajia kuleta mbegu bora za alizeti na kuzigawa kwa mkataba kwenye viwanda vinavyozalisha zao hilo hali itakafanya soko hilo kuwa la uhakika na kuondoa uhaba wa Mafuta unaojirudia kila Mwaka.
“Serikali itawajibika kwa kuwawezesha wakulima kwa kuwapelekea wataalamu wa zao la alizeti,na tutaweka masharti kuwa ukivuna alizeti unamuuzia mwenye kiwanda ili kuhakikisha viwanda vyote vinavyoingia mkataba vinazalisha mafuta kwa mwaka mzima,”amesema.
Pia Prof.Mkenda ametumia nafasi hiyo kuzitaka Benki zote nchini kutoa fursa ya mikopo kwa wakulima na kushusha riba ili kuchochea kilimo cha zao hilo ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wakulima wengi zaidi kukifanya Kilimo kuwa biashara.
“Ukitaka kupambana na umaskini Tanzaniana, unaweza kufanya mambo mengi Sana lakini ukweli ni kwamba umaskini utaaisha kwa kilimo,ukitaka mali utaipata shambani,”amesema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo Dkt.Tausi kida amesema kuwa changamoto za mitaji kwa wakulima nchini bado zipo nyingi na kwamba ipo haja kwa Taasisi za fedha kuongeza kiwango kwa wakulima.
“Ili kuweka tija kwenye Mazao ya kimkakati tunapaswa kuongeza nguvu Katika kukuza zao la alizeti na zabibu ili kusapoti viwanda vya uchakataji ,kwa upende wetu tumeanza na programu kwa mikoa ya Simiyu,Dodoma,Singida na Morogiro kwa Kutoa pembejeo,”ameeeleza
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amesema ili Kufanikisha maendeleo ya Kilimo Mkoani hapa inatarajia kusajili Kaya laki 3 zinazostahili kufanya kilimo biashara na kuwa fahari kwa jiji hili.
”Mazao ya zabibu na alizeti kuwa ya kimkakati ili Kufanikisha hilo nitatumia nafasi yangu kwa kushauriana na Wizara ya kilimo kuona namna ya kuongeza ufanisi kwa mazao hayo”amesema Mtaka