Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Nyasa Crodvic Duwe akikagua Mradi wa Kituo cha Afya Mbamba bay na Mradi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa katika Ziara ya Kamati ya Siasa ambayo imekagua miradi 4 na kuridhishwa na Utekelezaji wa miradi hiyo. (Picha na Ofisi ya Ded Nyasa.)
***********************
Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Nyasa, Jana imefanya ziara ya kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo 4 wilayani Hapa na kuridhishwa na maendeleo ya Miradi hiyo.
Miradi Iliyotembelewa ni Ujenzi wa Ujenzi wa Matundu Saba ya Vyoo na kuona jinsi huduma za afya zinavyotolewa kwa wananchi, katika Kituo cha Afya Mbamba Bay, Mradi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Nyasa, Mradi wa Maji Ukuli Kingerikiti, na Mradi wa Maji wa Kijiji cha Lundo Kata ya Lipingo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyasa Krodvic Duwe ambaye ni Mkuu wa Msafara wa Ziara hiyo amesema lengo la Ziara hiyo ni wajumbe waweze kutembelea na kukagua miradi ya Maendeleo ambayo inalenga kutatua changamoto za wananchi kwenye sekta za afya, Maji na Utawala.
Duwe katika Majumuisho ya Ziara hiyo, amesema kamati ya Siasa Wilaya ya Nyasa Imeridhishwa na kasi ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo, na kutoa pongezi kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Kanali Laban Thomas, Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa, Bw. Jimson Mhagama na Mbunge wa Jimbo la Nyasa kwa Kutekeleza Miradi hiyo kwa Ufanisi.
Akiwa katika Kituo cha afya Mbamba bay, alikagua ujenzi wa Vyoo wenye lengo la kutatua changamoto ya Upungufu wa Vyoo na kuridhishwa na hatua ya Utekeleza wake na kamati ilipata fursa ya kuongea na baadhi ya weagonjwa na wananchi, waliokuwepo maeneo ya Kituo cha afya na wakasema wanaridhishwa na huduma zinazotolewa na watumishi wa Afya, Kituo cha Afya cha Mbamba Bay, na kuupongeza uongozi wa Wilaya kwa kuboresha na kutoa Huduma Bora kwa Wananchi.
Katika Mradi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa, Kamati Pia Imeridhishwa na Ujenzi huo ambao umefikia hatua ya kukamilika kwa boma na Kumtaka Mh. Mbunge wa Jimbo la Nyasa kufuatilia kwa uKaribu Fedha za kumalizia Ujenzi .
Katika Miradi ya Maji ya Ukuli Kingerikiti kamati imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, na Wizara ya Maji kwa kutatua changamoto kubwa iliyokuwa inawakabili wananchi wa Ukuli Kingerikiti, kwa kutoa fedha za ujenzi na Ukarabati wa Mradi huo na kwa sasa wananchi hawana kero ya maji na wanafurahia huduma hiyo.
Katika Mradi wa Maji wa Kijiji cha lundo Kata ya Lipingo kamati imejionea kwa Dhati Serikali ilivyotatua kero ya maji katika Kata ya Lipingo mradi ambao utamaliza kero ya maji Katika Kata hiyo na imemtaka meneja wa RUWASA Mhandisi Evaristo Ngole, kusambasa maji hayo katika kata ya Lipingo na Liuli kwa kuwa maji ni Mengi yatakayokidhi walaji wa Kata ya Lipingo na ziada kubaki.
Ziara hiyo Imeambatana na Viongozi Wafufatao Mbunge wa Jimbo La Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, kanali Laban Thomas na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa Bw Jimson Mhagama.