Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stela Manyanya akikagua Mradi wa Maji katika Kijiji cha Lundo kata ya Lipingo Wilayani Nyasa jana.Aidha amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kutatua kero ya maji katika Kata ya Kingerikiti na Lipingo Wilayani Nyasa. (Picha na Ofisi ya Ded Nyasa.)
*******************************
Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya, amemshukuru na Kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kwa Kutekeleleza Miradi ya Maji Wilaya ya Nyasa.
Ameyasema hayo jana alipotembelea na kukagua miradi ya maji ya Ukuli, Kingerikiti na Mradi wa Kijiji cha Lundo, Kata ya Lipingo, Miradi ambayo imetatua kero ya wananchi wa kata ya Kingerikiti na Lipingo Wilayani Nyasa.
Mhandisi Manyanya amefafanua kuwa, Ukuli kingerikiti na Mradi wa maji wa Kijiji cha Lundo kata ya Lipingo ni Miradi ya maji ambayo ilikuwa ikimnyima usingizi kwa kuona wananchi walivyokuwa wakiteseka kuchota maji umbali mrefu lakini leo amefurahi kuona kero ya maji imekwisha, wananchi wakipata maji bombani.
Manyanya ameongeza kuwa anamshukuru kwa dhati Mh. Rais kwa sababu Serikali imempa fedha ya kutatua Kero ya maji ya katika kata hizo na Miradi mingine ikiwa inaendelea kutekelezwa, katika kijiji cha Likwilu na Ngingama ili kuendelea kutatua Kero ya Maji wilayani Nyasa.
Aidha amesema Wilaya ya Nyasa bado ina changamoto ya Upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo mengine hivyo bado anaomba asaidiwe miradi mingine ya maji katika Kata zilizobaki.
Aidha ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Nyasa kuitunza miundombinu ya maji iliyotengenezwa na Serikali na kuunga juhudi za Serikali kwa kuchangia gharama ndogo za ukarabati.