***************************
Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL Plc) na wadau wengine waliungana na wakulima wa Shahiri na mazao mengine wilayani Karatu mkoani Arusha kuadhimisha siku ya Wakulima wa Shahiri.
TBL kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kila mwaka huadhimisha Siku ya Wakulima inaoshirikiana nao, ambapo huweza kukutana nao kwa ajili ya kujua changamoto zinazowakabili pia huwakutanisha na wataalamu wa kilimo na sekta nyingine ambazo zinachangia kubadilisha maisha ya wakulima kuwa bora.
Kauli mbiu ya Siku hii mwaka huu ilikuwa ‘Wakulima wapatiwe Ujuzi ,Waunganishwe na wadau wa kufanikisha kazi yao na kuwapatia uwezeshaji wa kifedha’ ambayo na malengo endelevu ya kampuni mama ya ABInBEV ya kuinua wakulima wanaouzia malighafi viwanda vyake vlivyopo sehemu mbalimbali duniani.
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL,Bw.Jose Moran, alisema “Wakulima wadogo ni wadau wetu muhimu katika manunuzi yetu ya malighafi. kwani tunaamini katika kukuza mnyororo thabiti, endelevu na jumuishi”.
Alisema TBL Plc, imedhamiria kufanikisha Malengo Endelevu ifikapo 2025, lengo mojawapo likiwa kufanikisha kilimo cha kisasa. Katika kilimo kampuni imedhamiria kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2025 asilimia 100% ya wakulima wadogo inaoshirikiana wanapatiwa ujuzi, wanaunganishwa na wadau muhimu kufanikisha kazi yao na wanawezeshwa kifedha.
Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Abas Kayanda, alisema, “Kuboresha sekta ya kilimo nchini Tanzania, na uzalishaji wa shayiri, ni kipaumbele cha serikali. Matukio maadhimisho kama Siku ya Wakulima hutoa fursa ya kujenga uhusiano muhimu, kuwapatia wakulim aujuzi kutoka kwa wataalam,kutambua fursa na changamoto zinazowakabili”
Wakulima waliohudhuria siku hiyo walipata fursa ya mbinu za kilimo cha kisasa na kukutana na wadau mbalimbali wa tasnia ya kilimo. Maadhimisho haya ya kila mwaka yamekuwa sehemu muhimu katika kalenda ya kilimo nchini .