Mkuu wa Wilaya ya Nzega Kamishna Msaidizi wa polisi(ACP) Advera Bulimba (kushoto) akipokea leo Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Uyui Kisare Makori.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega Kamishna Msaidizi wa polisi(ACP) Advera Bulimba akiwa ameshika leo Mwenge wa Uhuru wakati wa kusoma Risala ya Utii ya wakazi wa Nzega kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakimbizi Mwenge wa Uhuru wakijadiliana jamb oleo kabla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi ujenzi wa ukumbi wa Serene uliopo Wilayani Nzega ambao hadi kukamilika utagharimu milioni 420.
Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru za mwaka 2021 Luteni Josephine Mwambashi (katikati) akitoa maagizo leo Mwekezaji wa ujenzi wa Ukumbi wa Serene kabla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi ya kuongeza kasi ya ujenzi huo ili uanze kutoka huduma kwa wananchi na Serikali iweze kupata mapato yake.
Kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru za mwaka 2021 Luteni Josephine Mwambashi (katikati) akiweka leo Jiwe la Msingi la ujenzi wa ukumbi wa Serene uliopo Nzega wakati wa mbio za Mwenge wa uhuru.
******************
NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
MAPATO katika Hospitali ya Wilaya ya Nzega yameongezeka kutoka milioni 99.1 mwaka 2019/20 hadi kufikia milioni 279.4 katika mwaka 2020/21 baada ya kuanza matumizi mfumo wa kuhifadhi taarifa za Kitabubu (GOTHOMIS).
Kauli hiyo imetolewa leo na Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO)ya Nzega Dkt.Jabil Juma wakati akitoa taarifa kwa Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru kuhusu mfumo wa kuhifadhi taarifa za Kitabubu (GOTHOMIS) ulivyosaidia kuongeza mapato.
Alisema walitumia kiasi cha shilingi milioni 25.5 kufunga mfumo ambapo mapato yalianza kupanda kutoka wastani wa shilingi milioni 9 hadi kufikia wastani wa milioni 23 kwa mwezi.
Dkt. Juma alisema hali imefanya kuwepo kwa ongezekoa la upatikanaji wa dawa muhimu kufukia asilimia 97.6.
Kwa upande wa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Luteni Josephine Mwambashi aliiagiza Wilaya ya Nzega kuhakikisha inaendelea kufunga Mfumo wa GOTHOMIS katika Zahanati na Vituo vya Afya kwa ajili ya kudhibiti upotevu wa fedha za umma katika maeneo mbalimbali.
Wakati huo huo Mwenge wa Uhuru umezindua miradi minne ya maendeleo ya sekta mbalimbali yenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni 1.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega Kamishna Msaidizi wa polisi(ACP) Advera Bulimba amesema kati ya fedha hizo Serikali kuu imechangia milioni 432.2, Wilaya imechangia milioni 219.1, wananchi wamechangia milioni 420 na wadau wa maendeleo wamechangia milioni 1.2.
Amesema katika mradi wa kwanza serikali imetoa kwa ajili ya ujenzi wa majengo mapya na ukarabati majengo ya zamani ya chuo cha Maendeleo ya Jamii Mwanhala kwa gharama ya milioni 432,mradi mwingine ni ufugaji wa mfumo wa GOTHOMIS katika Hospitali ya Wilaya kwa gharama ya milioni 25.5.
ACP Advera ameongeza kuwa mradi mwingine uliozinduliwa na Mwenge wa Uhuru ni wa uhifadhi wa mazingira ambao umegharimu milioni 12.5 , uwezeshaji wa vikundi vya Wajasiriamali ambapo zimetumia milioni 181 na kuwekwa kwa jiwe la msingi mradi wa sekta binafsi ambao unahusu ujenzi wa ukumbi kwa gharama ya milioni 420.