*****************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Klabu ya Yanga imeibuka na ushindi wa mbao 2-0 dhidi ya Ihefu Fc katika uwanja wa Benjamini MkapaJijini Dar es Salaam ambapo tulishuhudia kiungo wa klabu ya Yanga Feisal Salumu kupachika mabao yote mawili.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake na ullikuwa mchezo maalumu kwa klabu ya Yanga kumuaga Kiungo Mshambuliaji raia wa Rwanda Haruna Niyonzima ambapo mcehi hiyo kwake ilikuwa ni ya mwisho kwa klabu hiyo.
Feisal alipachika bao la kwanza dakika ya 17 ya mchezo katika kipindi cha kwanza na bao la pili alilifunga dakika ya 36 ya mchezo mara baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Kibwana Shomari.