Kiongozi wa Kitaifa wa mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru wa wa mwaka 2021 Luteni Josephine Mwambashi akitoa salamu za Mwenge wa Uhuru leo wilayani Sikonge Viongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wakikagua nyaraka mbalimbali leo za Ofisi ya Udhibiti Ubora wa Shule wilayani Sikonge wakati mbio maalumu.
Kiongozi wa Kitaifa wa mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru wa wa mwaka 2021 Luteni Josephine Mwambashi akizindua mradi wa usambazaji maji katiika Kijiji cha Kabanga wilayani Sikonge.
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge John Palimgo akipokea Mwenge wa Uhuru leo wakati wa salamu ya utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Picha na Tiganya Vincent
***************************
NA TIGANYA VINCENT
JUMLA ya miradi mitatu ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.1 Wilayani Sikonge imezinduliwa na Mbio maalum za Mwenge wa Uhuru mwaka 2021.
Miradi hiyo inajumuisha Sekta ya viwanda, elimu na Maji.
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge John Palingo alisema hayo jana wakati wa mbio hizo wilayani humo na kusema kati ya fedha hizo kiasi cha Shilingi milioni 37.8 ni mchango wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Shilingi bilioni 1.1 ni mchango wa Serikali Kuu, Wananchi wamechangia Shilingi laki 2.6.
Kauli mbiu ya mwaka huu ambayo inasema “TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu; Itumie kwa Usahihi na Uwajibikaji”.
Alisema katika mradi wa kwanza Mwenge wa Uhuru umeka Jiwe la Msingi ujenzi Kiwanda cha kuchakata mazao ya nyuki ambacho hadi kukamilika kitagharimu milioni 757.5.
Pallingo alisema kati ya fedha hizo Serikali kuu imechangia milioni 719 na Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge imechangia milioni 37.8.
Alisema mradi mwingine ni uzinduzi wa Jengo la Ofisi ya Udhibiti Ubora wa Shule ambao umegharimu jumla ya Shilingi milioni 152.
Alisema lengo la mradi huu lilikuwa ni kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa wathibiti ubora wa Shule zote za Msingi na Sekondari zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
Mkuu huyo wa Wilaya ya Sikonge umezinduzi wa mradi wa kusambaza maji ambao hadi kukamilika Shilingi milioni 245.3
Kiongozi wa Kitaifa wa mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru wa wa mwaka 2021 Luteni Josephine Mwambashi aliwataka Viongozi wa Wilaya ya Sikonge kuhakikisha wanaondoa mapungufu yote yaliyojitokeza.