Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.
Abdallah Ulega (Mb) akizungumza mara baada ya kufika katika Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuanza rasmi ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani
humo ambapo ameusisitiza uongozi wa mkoa huo kuwa na mkakati wa kumaliza
migororo ya wakulima na wafugaji ikiwemo njia ya kuhamasisha wafugaji kuvuna
mifugo yao na kuuza viwandani ili viwanda hivyo vipate malighafi kwa ajili ya
kuuza nyama ndani na nje ya nchi. (Picha
na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar
Kunenge akibainisha mikakati ya mkoa katika kumaliza migogoro ya wakulima na
wafugaji wakati Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega alipofika
ofisini kwake kabla ya kuanza rasmi ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo,
ambapo Mhe. Kunenge amewataka wakazi wa mkoa huo kutochukua sheria mkononi na
kuvielekeza vyombo vya ulinzi na usalama kutenda haki vinapopata taarifa juu ya
migogoro hiyo. (Picha na Edward Kondela,
Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.
Abdallah Ulega (Mb) akioneshwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya
Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi, sehemu ya eneo la Taasisi ya
Chanjo Tanzania (TVI) iliyopo Wilaya ya Kibaha, Mkoani Pwani ambalo limevamiwa na
baadhi ya wananchi na kujenga makazi. (Picha
na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.
Abdallah Ulega, (wa tatu kutoka kushoto) akioneshwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala
ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi moja ya mitambo
inayotumiwa na Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) iliyopo Wilaya ya Kibaha, Mkoani
Pwani. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo kutoka Wizara ya
Mifugo na Uvuvi Prof. Hezron Nonga. (Picha
na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.
Abdallah Ulega (Mb) akiangalia moja ya mitambo katika kiwanda cha kuzalisha chanjo
za mifugo cha HESTER kilichopo Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani na kusisitiza
chanjo zinazozalishwa nchini zinapaswa kufikishwa maeneo ya vijijini ili
wafugaji wakinge mifugo yao dhidi ya magonjwa mbalimbali. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari – Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Na. Edward Kondela
Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) ameusisitiza uongozi
wa Mkoa wa Pwani kutumia mkakati wa uvunaji wa mifugo kama mkakati wa
kumaliza migogoro ya wafugaji na wakulima pamoja na kuondokana na tatizo
la uhaba wa malighafi katika viwanda vya kuchakata nyama mkoani humo.
Naibu
Waziri Ulega amesema hayo leo (12.07.2021) alipokutana na uongozi wa
mkoa huo ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge,
wakati akitoa taarifa ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili Mkoani Pwani
na kufafanua kuwa ni vyema uongozi huo ukafanya tathmini ya kina kwa
kuunda kamati maalum ili kutafuta suluhu ya migogoro ya ardhi baina ya
wakulima na wafugaji mkoani humo.
Amesema viongozi ndani ya mikoa
yote nchini ni vyema wakaunda kamati maalum za wataalamu kwenda
wilayani hadi vijijini ili kutafuta ufumbuzi wa haraka na kudumu wa
kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji, ukiwemo mkakati wa
kuhakikisha wafugaji wanavuna mifugo yao kwa kuuza katika viwanda vya
kuchakata nyama ili vipate malighafi na kuuza nyama ndani na nje ya
nchi.
Mhe. Ulega amesema serikali inalichukulia suala hilo kwa
uzito mkubwa kwa kutumia kamati maalum kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Maji, Wizara ya Kilimo na Wizara ya
Mifugo na Uvuvi.
Amesema wizara ilishatuma timu ya kushughulikia jambo hilo kwa ngazi ya taifa na imetoka na mapendekezo kadhaa kwa hatua zaidi.
Mhe.
Ulega amesema Wizara ya Mifugo na Uvuvi inasisitiza mikoa kuunda kamati
ya wataalam kubaini mambo kadhaa ili kuchukua hatua ili jambo hilo
lisijitokeze katika maeneo mbalimbali nchini.
“Timu hizo
zitabaini maeneo ya mifugo vamizi, wafugaji wakorofi ili waweze
kuchukuliwa hatua kali sambamba na kubainisha mahitaji halisi ya
miundombinu ya mifugo, kuwepo kwa taarifa kamili za mifugo ilipo pamoja
na kuhamasisha kuwa na utamaduni wa kuuza mifugo kwenye viwanda vya
kuchakata nyama ili vipate malighafi.” amesema Mhe. Ulega
Akizungumzia
hali halisi ya hatua zilizochukuliwa na Mkoa wa Pwani kukabiliana na
kero hiyo mkuu wa mkoa huo Mhe. Abubakar Kunenge amewataka wakazi wa
Mkoa wa Pwani kutochukua sheria mkononi na kuviasa vyombo vya ulinzi na
usalama kutenda haki wanapopata taarifa ya migogoro hiyo.
Mhe.
Kunenge amefafanua kuwa mkoa huo tayari umeanza kufanya sensa ya mifugo
katika wilaya zote na Wilaya ya Rufiji kwa sasa ipo hatua za mwisho
kukabidhi mapendekezo yao.
Ameongeza kuwa taarifa hiyo ya sensa
wamebaini kuna wafugaji wengi waliopo katika wilaya hiyo hawajasajiliwa
na hawana taarifa zozote za wanakotoka wala wanakokwenda.
Katika
hatua nyingine Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akiwa
katika Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) iliyopo Wilaya ya Kibaha,
Mkoani Pwani ameagiza uongozi huo pamoja na wizara wanaohusika na
masuala ya chanjo kuhakikisha chanjo zinazozalishwa na taasisi hiyo
zinawafikia wafugaji waliopo vijijini badala ya kuanza kufikiria
kusambaza chanjo hizo nje ya nchi.
Mhe. Ulega amesema kuna mifugo
mingi kama kuku, ng’ombe na mbuzi wanaokufa kwa kuwa wafugaji hawajui
kama kuna chanjo zinazozalishwa hapa nchini ingawa kuna maeneo mengine
chanjo hizo hazijafika kabisa.
Ametaka viongozi hao kuhakikisha
chanjo zinafika maeneo mbalimbali nchini hususan maeneo ya vijijini ili
wafugaji waweze kukinga mifugo yao dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Mhe.
Ulega ametembelea pia kiwanda cha kuzalisha chanjo za mifugo cha HESTER
kilichopo Wilayani Kibaha na kujionea namna kiwanda hicho kikiwa tayari
kuanza kuzalisha chanjo ambazo zitakuwa zikiuzwa ndani na nje ya nchi.
Akiwa
kiwandani hapo ameendelea kusisitiza chanjo za mifugo kufikishwa maeneo
mbalimbali nchini hususan ya vijijini ili mifugo iwe na afya bora na
wafugaji waweze kunufaika kupitia ufugaji