Maafisa wa Wakala wa Vipimo (WMA) wakihakiki matenki ya kuhifadhi mafuta.
Roli la mafuta likihakikiwa katika Kituo cha Wakala wa Vipimo (WMA) Misugusugu Mkoa wa Pwani.
**************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Wakala wa Vipimo (WMA)wanawajibu wa kuzihakiki flow meter za kwenye mabomba yanayotiririsha mafuta kutoka kwenye meli ili ziwe na usahihi na zinapokuwa na usahihi Serikali inaweza kupata kodi stahiki.
Ameyasema hayo leo Meneja Kitengo cha Bandari (WMA), Bw.Peter Chuwa katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere kwenye Viwanja vya Mwalimu Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa mafuta yanapotoka kwenye flowmeters huwa yanaenda kwenye matenki makubwa ya kuhifadhia mafuta ambayo ni maghala na yale maghala nayo ni vipimo na kile kipimo kina hakikiwa na wakala wa vipimo.
“Mafuta yanapotoka kwenye matenki makubwa yanapouzwa kwenye maroli au matenki yaliyopo kwenye maroli yale matenki pia huwa yanahakikiwa na Wakala wa Vipimo, ili yule mwenye ghala anapouza mafuta yake kwenye maroli aweze kuwa na uhakiki kwamba kile kipimo kimehakikiwa na wakala wa vipimo na kiko sahihi”. Amesema Bw.Chuwa.
Aidha amesema maroli yanapopeleka mafuta kwenye visima vya chini (ardhini) zile tanki za ardhini pia huwa zinahakikiwa na Wakala wa vipimo ili anaposhusha mafuta yule mmliki wa kituo cha mafuta aweze kupata mafuta yake stahiki kutoka kwenye roli
“Zile petrol Pampu zilizopo kwenye vituo vya mafuta nazo zinahakikiwa na wakala wa vipimo kila mara ili unapokuja na gari yako unapotoa fedha zako ili huuziwe mafuta ziwe sahihi na kiasi unachotaka”. Ameeleza Bw.Chuwa