Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka akisalimiana na Wajasiriamali Wanawake wanaojishughulisha na biashara ya kuuza ndizi katika soko la Lembuka Tandale, Kiwira Wilaya ya Rungwe ikiwa siku ya kwanza ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM na Sekretarieti ya CCM Taifa mkoani Mbeya leo Julai 11, 2021.(Picha na CCM Makao Makuu)
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka akizungumza na wakazi wa shina namba 6 kwa Balozi Said Mwakisisile, Kata ya Bagamoyo, Tarafa ya Tukuyu Wilaya ya Rungwe ikiwa siku ya kwanza ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM na Sekretarieti ya CCM Taifa mkoani Mbeya leo Julai 11, 2021.(Picha na CCM Makao Makuu)
******************************
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka akizungumza na wakazi wa Shina namba 1, Tawi la Msapania kata ya Chapwa ,Tunduma wilaya ya Momba ikiwa sehemu ya hitimisho ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM na Sekretarieti ya CCM Taifa mkoani mkoani Songwe.
Katika kikao hicho kwa Ndugu Shaka aliwaeleza wakazi wa eneo hilo kuwa ushindi wa CCM unatokana na mfumo mzuri ulioanzia ngazi ya Shina mpaka Taifa.
“CCM tutaendelea kushinda na kushinda kwa sababu mfumo tuliojiwekea unaeleweka, unajipambanua, na ni mfumo ambao baada ya ushindi huu tuna andaa ushindi ujao” alisema Shaka.
Ziara hizi za Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo na Sekretarieti ya CCM Taifa ina lengo la kukagua na kuhamasisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 ambapo pamoja na mambo mengine Viongozi wa CCM Taifa wameshuka chini na kufanya vikao na Mabalozi wa Shina na wananchi wao ikiwa sehemu ya kutambua mchango mkubwa wa Mabalozi na kusikiliza kero zinazowagusa wananchi wa eneo husika.