*******************
Na Penina Malundo
MAMLAKA ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA), imewataka wakulima wa zao la mpunga kuacha kulima kizamani na badala yale kutumia teknolojia za kisasa katika ulindaji wa mashamba yao ili kuona tija ya zao hilo.
Akizungumza katika maonesho ya 45 ya biashara ya kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere maarufu (Sabasaba), Mtaalamu wa somo la umeme kutoka VETA Mikumi, Jones Hokororo amesema, teknolojia hiyo imekuja kubadilisha muonekano wa ulindaji wa mazao hayo kama wakulima kuamia na familia zao mashambani.
Amesema, teknolojia hiyo ikiwa inafanya kazi inakuwa inatoa sauti ya milio ya ndege na kuwafukuza ndege kufika katika mazao.
“Ni moja ya teknolojia nzuri kwa wakulima wa Mpunga na nafaka katika kufanya mazao ya wakulima kutoliwa na wadudu hao,”amesema
Hokororo amesema kutokana na changamoto kwa wakulima hao kuamia na familia shambani na kushindwa kufanya majukumu mengine VETA imeamua kuja na ufumbuzi wa teknolojia hiyo.
“Unakuta mtu anashindwa kufanya mambo mengine nahamia shambani kisa kufukuza ndege sasa teknolojia hii itaweza kuwarahisishia kwa urahisi kazi zao,”.
“Sisi kama Veta tumeona kuna kila sababu ya kutengeneza kifaa cha kufukuzia ndege ambacho kina ita kwa milio mitatu tofauti kama Tai,kipanga pamoja na mwewe ambapo ndege wakisikia mlio huu wanakimbia,”amesema Hokororo.
Aidha amesema matumizi ya kifaa hicho mbali ya kusaidia wakulima pia ni rafiki kwa mazingira kwani hakichafui mazingira.