****************************
Happy Lazaro, Arusha.
Arusha.Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha,linamshikilia Melita Ndaletyan(34) kwa tuhuma za kumuua kaka yake Kiseri NdaIetyan ( 38),baada ya marehemu kumzuia mtuhumiwa aliyekuwa akitaka kumwingilia kimwili mke wa kaka yao mkubwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha leo,Justine Maseju,alisema tukio hilo lilitokea Julai 8 2021 majira ya saa 6:30 usiku,katika Kitongoji cha Naamalasin,Kata ya Noondoto wilayani Longido mkoa wa Arusha.
Alidai kuwa Kiseri alifariki dunia baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni na mdogo wake ambapo wote wawili ni wafugaji ambapo ndugu wote watatu wanaishi kwsnyw boma moja na kuwa siku ya tukio mtuhumiwa alitaka kutenda kosa hilo kwa mke wa kaka yake ambaye hakuwepo nyumbani wakati huo.
Kamanda amesema kwa mujibu wa uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni tamaa ya kimapenzi ambapo mtuhumiwa huyo anadaiwa kutaka kumwingilia kimwili mke wa kaka yake na kuzuiwa na marehemu kufanya jambo hilo jambo lililosababisha ugomvi kati yao.
“Mtuhumiwa,marehemu pamoja na kaka yao mwingine wote walikuwa wanaishi kwenye boma moja hivyo mtuhumiwa wakati anataka kumwingilia kimwili mke wa kaka yake(mkubwa) ambaye hakuwepo nyumbani,marehemu alitokea na kumkataza kufanya hivyo ndipo mtuhumiwa alimchoma na kitu chenye ncha kali,”
“Jeshi la Polisi linaendelea kumshikilia mtuhumiwa kwa kumfanyia ukatili ndugu yake na mara baada ya upelelezi kukamilika jalada litapelekwa Ofisi ya mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria,”
Kwa mujibu wa Kamanda mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa familia kwa ajili ya taratibu za maziko baada ya mwili huo kufanyiwa uchunguz
Wakati huo huo mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka minne alikutwa akiwa ametelekezwa Julai 6 mwaka huu majira ya saa 6 mchana katika maeneo ya Burka,Kata ya Olasiti jijini Arusha.
Kamanda huyo amedai kuwa mtoto huyo ambaye jina lake pia linahifadhiwa ni mkazi wa eneo la Majengo.
“Taarifa za awali zilibaini kwamba mtoto huyo alifanyiwa ukatili wa kipigo pamoja na kuwekewa majani mdomoni na baba yake wa kufikia na Jeshi la Polisi liliendelea na upelelezi na kubaini kwamba, kuna mgogoro wa kifamilia kati ya mama wa mtoto huyo na baba wa kufikia (jina linahifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi),”amesema
“Mara baada ya kufanya tukio hilo mtuhumiwa alikimbia na Jeshi la Polisi mkoani hapa tulifanya jitihada za kumtafuta kwa kushirikiana na raia wema na kufanikiwa kumkamata.Nitoe
wito kwa wananchi kutoa taarifa dhidi ya ukatili na unyanyasaji wa watoto kwa Jeshi la Polisi ili kukomesha au kumaliza kabisa tatizo la unyanyasaji kwa watoto,”
Aidha kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na baadhi ya mashuhuda waliomkuta mtoto huyo katika eneo hilo walidai kuwa aliwaeleza kuwa amefanyiwa ukatili(kulawitiwa)na baba yake wa kufikia.
“Kuhusu hizo taarifa za mtoto kulawitiwa na baba yake wa kufikia tunazo na amefanyiwa ukaguzi na wataalam ambao bado wanaendelea kumfanyia uchunguzi mtoto ila hadi sasa inaonekana tendo hilo halikuweza kufanyika,”alidai Kamanda huyo.