Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako akizungumza katika hafla ya kukabidhi rasmi vifaa vya kufundishia kozi za uhandisi wa matengenezo ya ndege (Aircraft Maintenance Engineer) kwaajili ya shule kuu ya masuala ya anga Chuo cha Usafirishaji (NIT) vilivyonunuliwa kwa ufadhili wa Serikali kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamia na Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA).
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT (NIT) Prof. Blasius Nyichomba akizungumza katika hafla ya kukabidhi rasmi vifaa vya kufundishia kozi za uhandisi wa matengenezo ya ndege (Aircraft Maintenance Engineer) kwaajili ya shule kuu ya masuala ya anga Chuo cha Usafirishaji (NIT) vilivyonunuliwa kwa ufadhili wa Serikali kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamia na Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA).
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)Prof.Zacharia Mganilwa akizungumza katika hafla ya kukabidhi rasmi vifaa vya kufundishia kozi za uhandisi wa matengenezo ya ndege (Aircraft Maintenance Engineer) kwaajili ya shule kuu ya masuala ya anga Chuo cha Usafirishaji (NIT) vilivyonunuliwa kwa ufadhili wa Serikali kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamia na Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA).
akizungumza katika hafla ya kukabidhi rasmi vifaa vya kufundishia kozi za uhandisi wa matengenezo ya ndege (Aircraft Maintenance Engineer) kwaajili ya shule kuu ya masuala ya anga Chuo cha Usafirishaji (NIT) vilivyonunuliwa kwa ufadhili wa Serikali kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamia na Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA).
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako akimsikiliza Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)Prof.Zacharia Mganilwa katika hafla ya makabidhiano ya vifaa vya kufundishia kozi za uhandisi wa matengenezo ya ndege (Aircraft Maintenance Engineer) kwaajili ya shule kuu ya masuala ya anga Chuo cha Usafirishaji (NIT) vilivyonunuliwa kwa ufadhili wa Serikali kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamia na Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA).
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako akikata utepe kuashiria makabidhiano ya vifaa vya kufundishia kozi za uhandisi wa matengenezo ya ndege (Aircraft Maintenance Engineer) kwaajili ya shule kuu ya masuala ya anga Chuo cha Usafirishaji (NIT) vilivyonunuliwa kwa ufadhili wa Serikali kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamia na Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA).
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako akipata picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa elimu nchini katika hafla ya kukabidhi rasmi vifaa vya kufundishia kozi za uhandisi wa matengenezo ya ndege (Aircraft Maintenance Engineer) kwaajili ya shule kuu ya masuala ya anga Chuo cha Usafirishaji (NIT) vilivyonunuliwa kwa ufadhili wa Serikali kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamia na Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA).
************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako amekabidhi rasmi vifaa vya kufundishia kozi za uhandisi wa matengenezo ya ndege (Aircraft Maintenance Engineer) kwaajili ya shule kuu ya masuala ya anga Chuo cha Usafirishaji (NIT) vilivyonunuliwa kwa ufadhili wa Serikali kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamia na Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA).
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo, katika chuo cha NIT jijini Dar es Salaam, Prof. Ndalichako amesema mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya sita ni kuwekeza katika mafunzo ya kuongeza ujuzi na ambayo yatasaidia kutatua changamoto zinazokabili jamii.
“Serikali imekuwa ikihimiza Vyuo vyetu Vikuu vihakikishe kwamba wanafunzi wanafanya mafuynzo zaidi na pia kuanzisha programu nyingine ambazo zinalenga kuwajenea wanafunzi ujuzi na ujuzi ambao unahitajika kwenye viwango vya kitaifa na hata viwango vya kimataifa”.Amesema Prof.Ndalichako.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha NIT Profesa Zacharia Mganilwa amemuomba Professa Ndalichako kuwasaidia kupata vifaa vya kufundishia wataalamu wa reli ambapo kwa sasa ndiyo wameanza kutoa mafunzo hayo.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa TEA, BI Bahati Geuzye amesema taasisi yake itaendelea kushirikiana na taasisi za elimu nchini ikiwa ni pamoja na NIT ili kuendelea kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia kwa lengo la kuongeza ubora wa elimu na upatikanaji wake kwa usawa.
Amesema kupitia ufadhili huo vijana wengi wa kitanzania wenye ndoto za kuwa wataalamu katika sekta ya usafiri wa anga watafikia ndoto zao kwa kupata masomo yao hapa hapa nchini kwa gharama nafuu.
“Ufadhili wa vifaa hivi utasaidia sana utoaji wa mafunzo katika uhandisi wa matengenezo ya ndege, taaluma ambayo ni muhimu katika kufanikisha jitihada za Serikali za kupiga hatua zaidi za kiuchumi”. Amesema Bi.Geuzye.