WAZIRI wa Maji Mhe.Jumaa Aweso,akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha watendaji wa wizara ya maji na taasisi zake katika kada ya manunuzi na ugavi, uhasibu na wakaguzi wa ndani kilichofanyika leo Julai 8,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Maji Mhe.Jumaa Aweso,akisisitiza jambo kwa washiriki wakati kikao kazi cha watendaji wa wizara ya maji na taasisi zake katika kada ya manunuzi na ugavi, uhasibu na wakaguzi wa ndani kilichofanyika leo Julai 8,2021 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba,akizungumza wakati wa kikao kazi cha watendaji wa wizara ya maji na taasisi zake katika kada ya manunuzi na ugavi, uhasibu na wakaguzi wa ndani kilichofanyika leo Julai 8,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi Clement Kivegalo,akizungumza wakati wa kikao kazi cha watendaji wa wizara ya maji na taasisi zake katika kada ya manunuzi na ugavi, uhasibu na wakaguzi wa ndani kilichofanyika leo Julai 8,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso,(hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha watendaji wa wizara ya maji na taasisi zake katika kada ya manunuzi na ugavi, uhasibu na wakaguzi wa ndani kilichofanyika leo Julai 8,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa kitengo cha Manunuzi Dkt.Christopher Nditi,akizungumza wakati wa kikao kazi cha watendaji wa wizara ya maji na taasisi zake katika kada ya manunuzi na ugavi, uhasibu na wakaguzi wa ndani kilichofanyika leo Julai 8,2021 jijini Dodoma.
Mhasibu wa RUWASA Mkoa wa Geita Bi.Zuwena Ally,akielezea changamtoto walizonazo wakati wa kikao kazi cha watendaji wa wizara ya maji na taasisi zake katika kada ya manunuzi na ugavi, uhasibu na wakaguzi wa ndani kilichofanyika leo Julai 8,2021 jijini Dodoma.
Mhasibu wa RUWASA mkoa wa Dodoma Bw.Isihaka Mwanjali,akitoa maoni yake wakati wa kikao kazi cha watendaji wa wizara ya maji na taasisi zake katika kada ya manunuzi na ugavi, uhasibu na wakaguzi wa ndani kilichofanyika leo Julai 8,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Utawala Barnabas Ndunguru akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki kwa Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso,(hayupo pichani) mara baada ya kufungua kikao kazi cha watendaji wa wizara ya maji na taasisi zake katika kada ya manunuzi,ugavi, uhasibu na wakaguzi wa ndani kilichofanyika leo Julai 8,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akiwa katika picha ya pamoja na watendaji Wakuu wa Wizara yake na baadhi ya Watendaji wa kada za Uhasibu, Uafisa Ugavi na Wakaguzi wa ndani mara baada ya kufungua kikao kazi cha pamoja leo Julai 8,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma.
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amemsimamisha kazi Afisa Ugavi wa Bonde la ziwa Tanganyika Mkoani Kigoma Victor Kaphipa kwa kosa la kufanya udalali ndani ya wizara hiyo na kuichafua taswira.
Agizo hilo amelitoa leo Julai 8,2021 jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha watendaji wa wizara ya maji na taasisi zake katika kada ya manunuzi ,ugavi, uhasibu na wakaguzi wa ndani chenye lengo la kusikiliza changamoto wanazokutana nazo katika utendaji wao.
Mhe.Aweso amesema wizara hiyo haina mashamba wala viwanja hivyo hakuna haja ya kuwa na watumishi ambao ni madalali wa wakandarasi wanaoomba kazi katika wizara hiyo.
“Kuna watu kwenye wizara ya maji wamekuwa madalali,yaani yeye ndio waziri,naibu waziri,katibu mkuu,naibu katibu mkuu yaani anafanya robbing,nataka niwaambie kama mnaona ni masihara kuna mtu anaitwa Kaphipa,yeye si dalali wa wizara ya maji nataka asimame,yupo wapi asimamame,yaani alipangiwa Kigoma hata ofisini hajaripoti,huyu anachafua wizara,naomba mmsimamishe huyu sitaki kumuona katika wizara yetu ya maji,”Aweso
Aweso amewataka watumishi hao kwenda kufanya kazi kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu zilizowekwa huku akiwasisitiza zaidi kutenda haki,kuzingatia nidhamu na kuboresha mahusiano mazuri katika utekelezaji wa majukumu yao.
‘’Pasipo na nidhamu mipango mizuri haiwezi kufanikiwa nidhamu ianze kwa mtu mmoja mmoja, dhamira yetu kwenye wizara ya maji ni kuhakikisha miradi ya maji itekelezwe kwa ubora na kumalizika kwa wakati”amesema Aweso
Pia Aweso amesema kuwa ukiacha Bajeti ya sh Bilion 680 waliopewa na Serikali,Rais Samia amewaongezea sh billion 207 ili kuboresha sekta ya Maji kwa sababu ameipa kipaumbele.
‘’Tusishangilie tu kuwa tumeongezewa fedha halafu mkajenge mianya ya kutumia fedha vibaya,hizi fedha haziliki ,ukiamua kula kwa makusudi hizi fedha za mama Samia jela inakuita’’amesisitiza Aweso
Awali Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Nadhifa Kemikimba ameelezea umuhimu wa kikao hicho katika kuboresha utendaji kazi wao na kuwasisitiza kushiriki kikamilifu
”Nakupongeza Waziri kutokana na utendaji kazi unaoufanya hivyo sisi kama watendaji wako hatutakuangusha na yote ulituambia tutaendelea kuyatekeleza kwa vitendo ”amesema Mhandisi Kemikimba