Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akitazama moja ya ubunifu uliofanya na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mara baada ya kuembelea banda la Chuo hicho katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akizungumza na baadhi ya wanafunzi wabunifu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mara baada ya kuembelea banda la Chuo hicho katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akitazama moja ya ubunifu uliofanya na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mara baada ya kuembelea banda la Chuo hicho katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Kipanga Juma Omary (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof.William Anangisye mara baada ya kuembelea banda la Chuo hicho katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akipokea zawadi kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof.William Anangisye mara baada ya kuembelea banda la Chuo hicho katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa leo jijini Dar es Salaam.
*****************************
NA EMMANUEL MBATILO
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako amekipongeza Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuendeleza bunifu ambazo zinalenga moja kwa moja kutatua changamoto katika jamii.
Ametoa pongezi hizo leo mara baada ya kutembelea banda la COSTECH katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa leo jijini Dar es Salaam.
Amesema Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimekuwa ikikiendeleza wabunifu ambao wamekuwa chachu ya kusaidia changamoto ambazo jamii zetu zimekuwa zikikumbana nazo hasa kwenye suala la ajira.
“Nimefurahi kuona kwamba zile nadharia ambazo zinafundishwa zinaenda mbali wanaweza kufanya vitu kwa vitendo ambavyo moja kwa moja vinaenda kugusa katika kujenga ujuzi unaomwezesha mtu kujiajiri au kuajiriwa katika sekta ambazo zinagusa changamoto za Watanzania”. Amesema Prof.Ndalichako.
Aidha Prof.Ndalichako ametoa wito kwa wabunifu ambao wamekuwa na changamoto ya kimasoko hivyo atashirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara kuona ni namna gani wanaweza kuwasaidia katika kuwatangazia biashara zaidi ili waweze kupata wateja na biashara na ubunifu wao uweze kwenda kutoa mchango kwenye taifa letu.