*****************************
Na Alex Sonna,Dodoma
TAKUKURU Mkoa wa Dodoma imefanikiwa kuokoa na kudhibiti zaidi ya shilingi milioni 200 ambazo zingepotea kwa kuchepushwa kufujwa ama kulipwa kwa watu wasiostahili kinyume na utaratibu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Julai 2,2021,Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo amesema ufuatiliaji wa Takukuru Mkoa wa Dodoma umewezesha kudhibiti fedha hizo ambazo zilitakiwa kulipwa kinyume cha utaratibu.
Kamanda Kibwengo ametolea mfano wa uchepushaji wa gari la Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma ambalo lilipata ajali na kupelekwa gereji moja Jijini Dodoma ambapo ilibaini vifaa 101 vyenye thamani ya shilingi milioni 87,785,000 vilichepushwa kutoka kwenye gari hilo.
“Kwa kushirkiana na Temesa ikabainika kwamba vifaa 101 vyenye thamani ya sh.87,785,000 vilichepushwa kutoka kwenye gari hilo hadi tulipoingilia na kuwezesha vifaa hivyo kurejeshwa,”amesema.
Mkuu huyo wa Takukuru Mkoa wa Dodoma amewataka wamiliki wa gereji binafsi mkoani dodoma wenye tabia ya kuchepusha na kubadilu vipuli vya magari ya umma wanayoletewa kwaajili ya matengenezo waache tabia hiyo kwani wanafatilia na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakao bainika.
Aidha, Kibwengo amesema kuwa miradi 20 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi 1,775,763,746 katika sekta ya elimu,afya na ujenzi ilikaguliwa kwa lengo ka kujiridhisha iwapo thamani halisi ya fedha imepatikana kwa kuangalia iwapo kuna ufujaji.
Amesema miradi 19 imebainika kutekelezwa kwa kiwango stahiki lakini wamebaini uchepuzi wa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya sh.41,850,000 kwenye mradi mmoja na wanafuatilia ili vifaa hivyo virejeshwe mara moja
“Ufuatiliaji wetu umewezesha kuokoa na kudhibiti jumla ya sh.215,660,000 ambazo zingepotea kwa kuchepushwa,kufujwa au kulipwa kwa watu wasio stahili kinyume nataratibu,”amesema.
Amesema kuwa sekta nyingine ni za binafsi asilimia 7,Elimu,Afya na Polisi asilimia 6 kila moja.
Hata hivyo amewataka watumishi waliopo katika sekta zinazolalamikiwa zaidi kwa rushwa katika mkoa wa dodoma kujitafakari kwani siku za mwizi ni arobaini.
Pia, amesema kuwa wamefanya chambuzi 6 za mifumo ya utendaji na utoaji huduma katika sekta za ardhi,elimu,mapato na ujenzi ambapo mianya ya rushwa ilibainishwa.
“Baadhi ya chambuzi zilizofanyika ni rushwa na udanganyifu katika mitihani katika baadhi ya vyuo ambapo imebainika kuna baadhi ya wahadhiri na watumishi wengine wa vyuo wanashirikiana na wanafunzi kufanya udanganyifu katika mitihani”,”amesema.
Vilevile,amesema uchambuzi wa mfumo wa kudhibiti mianya ya rushwa katika minada ulibaini kwamba zaidi ya asilimia 150 ya mapato kwenye minada hiyo yanapotea kwa nyia ya rushwa.
Amesema kuwa wanaendelea kuwataka wananchi kufatilia elimu wanazotoa ili kuyafahamu vizuri makosa ya rushwa kwa mujibu wa sheria ili kwa siku za usoni watoe taarifa zinazohusu vitendo vya rushwa.
Katika hatua nyingine,Kibwengo amesema kuwa majalada 20 ya uchunguzi yalikamilika na mashauri mapya yalifunguliwa mahakamani.
“Uchunguzi wa taarifa zingine unaendelea ukiwemo wa watu ambao wameghushi nyaraka za umiliki wa eneo la hifadhi ya msitu wa Isabe lililoko wilayani Kondoa mahali ulipo mnara wa kampuni moja ya simu na hivyo kwa takribani miaka 12 wameweza kujipatia shilingi ml.70 kwa njia ya udanganyifu,”amesema.
Amesema kitendo hicho ni kosa chini ya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa sura ya 329 marejeo ya mwaka 2019.
Amesema tayari wamefanikiwa kumpata mtuhumiwa mmoja ambaye anaendelea kusaidia uchunguzi ili kuwapata wenzake ambapo amedai kwa sasa wamezuia malipo ya mnara huo kwa mujibu wa sheria ili malipo yalipwe kwa mmiliki halali wa eneo ambaye ni halmashauri ya wilaya ya kondoa.
Mkuu huyo wa Takukuru Mkoa wa Dodoma amesema katika robo ya Julai hadi septemba 2021 wanatarajia kuweka msisitizo katika uelimishaji wakati wa mbio maalum za mwenge na kwa makundi hasa ya vijana na watendaji wa mitaa na vijiji.
“Pia tumejipanga kufatilia utekelezaji wa maendeleo haya ile ya kimkakati pamoja na yase