Wanachama wa Yanga wamekubali rasmi kuingia katika mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji na mabadiliko ya katiba kwenye mkutano mkuu uliofanyika leo June 27,2021 jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla aliwauliza wanachama kuhusu kuafiki mabadiliko hayo mara baada ya kutambulisha kamati iliyosimamia mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji.
Wajumbe waliopitisha mabailiko ni 1170 ambao walijiandikisha katika Mkutano Mkuu wa Yanga katika ukumbi wa DYCC.
Dk Msolla amesema idadi hiyo baada ya wanachama hao kupitisha mabadiliko kwa kura za ndio .
Baada ya Dk Msolla kuwauliza wanachama wanaoafiki mabadiliko hayo na ukumbi mzima ukanyoosha mikono akiwamo mgeni rasmi, Rais wa awamu ya nne, Dk Jakaya Kikwete huku baadhi yao wakipiga kelele kuwa wote wanaafiki.
Baada ya hatua hiyo, Dk Msolla aliwakabidhi vyeti wajumbe wa kamati hiyo na kisha akarejea tena kwa wanachama kuwauliza wasiohafaki na hakuna mkono ulionyooshwa.
Sehemu ya mabadiliko kwa klabu ya Yanga ni kuifanya timu hiyo kuwa kampuni huku klabu ikimiliki hisa aslimia 51 na wawekezaji wakimiliki hisa asilimia 49.