****************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Klabu ya Simba Sc yuaendelea kuunyemelea ubingwa wa ligi kuu bara mara baada ya leo kuinyoosha Mbeya City mabao 4-1 kwenye uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Simba Sc imeonesha dhahiri kwamba ubingwa ubaki kwa wekundu hao hasa kwa kuonesha kandanda safi uwanjani huku ikiwa na shauku ya kuondoka na ushindi mnono kwa kila mechi.
Kwenye mchezo wa leo Simba ilitengeneza nafasi nyingi za mabao angali ilifanikiwa kupoachika mbao 4-1 ndani ya dakika 90 za mchezo.
Mabao ya Simba Sc yalifungwa na Bwalya dakika 31, Miquissone 35, Bocco 47 na Chama 85 huku bao la kufutia machozi la Mbeya City likifungwa na Athanas 51.