Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA), Bw.Tumaini Nyamhokya akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama Mkoa wa Dar es Salaam ambao umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Lamada leo Jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa Chama cha wafanyakazi wa serikali za Mitaa Tanzania (Talgwu) wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Chama Mkoa wa Dar es Salaam ambao umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Lamada leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (Talgwu) Bw. Rashid Mtima akizungumza Mkutano Mkuu wa Chama Mkoa wa Dar es Salaam ambao umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Lamada leo Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
***************************
Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA), Bw.Tumaini Nyamhokya amesema mpaka sasa chama kimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kinafuata Demokrasia na wanapowachagua viongozi ambao wataiwakirisha vyema mikoa na kusikilizana wanaamini vyama vyao vitakuwa imara.
Ameyasema hayo leo akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa(TAWLGU) mkoa wa Dar es Salaam ambao unaendana na uchaguzi wa viongozi wa Mkoa huo.
Akizungumza katika mkutano huo Bw.Nyamhokya amesema kuwa ni vema viongozi kukaa meza moja huku wakiimba wimbo mmoja ambao watakubaliana kwa hoja bila kwenda kwenye migomo au kuingia barabarani.
Aidha Bw.Nyamhokya amesema kuingia kwenye migomo au kuingia barabarani hawajazuiliwa ila kukaa mezani na kujadiliana kwa pamoja kupata ufumbuzi wa mambo yao na mafanikio mengi kutafanya uwepo wa kusikilizana baina ya viongozi wa Taifa na Chama ambapo watavyama vitakuwa imara zaidi.
“Ni jambo jema Chama cha wafanyakazi kufanya uchaguzi wa kidemokrasia kama huu kwani mkoa wa Dar es Salaam ni mkubwa ambao umegawanyika kwa Mikoa ya Kinondoni, Ilala na Temeke kwa mujibu wa matakwa na kanuni za Chama cha TAWLGU,”Amesema Bw.Nyamhokya.
“Tunatarajia leo watapatikana viongozi wazuri ambao watakiongoza Chama vizuri na watakaosikilizana na kuimba wimbo mmoja ambao watakubaliana kwa hoja na kufanya wa Chama kutakuwa imara zaidi,”aAmesema .
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TAWLGU ,Bw.Rashid Mtima amesema kuwa wamekusanyika kwenye Mkutano Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ambapo kikatiba kikao hicho ni kikao ambacho kinajumuisha wajumbe wote wa mkoa wa Dar es Salaam wanaotoka katika Matawi.
“Kikao hiki kufanyika kikatiba kila baada ya miaka mitano lengo lake ni kupitia taarifa za Chama za kazi na kifedha kwa miaka mitano iliyopita ,leo watakaa na kupitia ripoti ya miaka mitano katika Mikoa wa Dar es Salaam pia wataweka Uongozi wa miaka mingine mitano ambapo watachagua Mwenyekiti wa mkoa wa Dar es Salaam,”Amesema Bw.Mtima
“Katiba imeipa Mamlaka Chama kuanzisha mkoa tangu mwaka jana ambapo baraza kuu liliidhinisha Mikoa mitatu ya Dar es Salaam iianzishwe ikiwemo mkoa wa Temeke,ilala na Kinondoni hivyo leo wanafanya uchaguzi wa mkoa wa Dar es Salaam lakini wakitoka hapa wataenda kuchagua viongozi wa Mikoa mitatu ilihuduma kwa wanaachama ifike vizuri katika kuwahudumia,”Amesema.
Hata hivyo Bw.Mtima amesem kanuni za Chama za mwaka 2018 zinazungumza kwamba pindi viongozi wakichaguliwa wanapaswa kupewa mafunzo ya uongozi ya shughuli za Chama hivyo viongozi watakaochagulia watapewa mafunzo ya Uongozi kwa shuguli za Chama cha wafanyakazi.