**********************************
Serikali imeshauriwa kuwekeza fedha katika kufanya utafiti na ugunduzi Mbalimbali kwani Tanzania ina watu wenye uwezo mkubwa wa kufanya mambo kama Mataifa mengine yaliyoendelea.
Ushauri huo umetolewa jijini Dar es salaam na Profesa Wa masuala ya kale Felix Chami wakati akizungumza katika hafla ya fupi ya kumtambua kuwa profesa kamili, mara baada ya kufanya utafiti wa mambo ya kale juu ya watu waliokuwepo kipindi cha nyuma hapa nchini Tanzania.
Amesema kuwa vijana wa kitanzania na wakiafrika kiujumla wana uwezo wa kufanya mambo makubwa na kugundua bidhaa ambazo zinauwezo wa kuwa na ubora zaidi .
Aidha ameiomba serikali kuboresha miundombinu katika shule za sekondari mpaka vyuo vikuu ikiwemo kuwa na vifaa bora vya kufundishia ili kuandaa wajuzi wa kutosha ambao watafanya Tanzania kuwa na vitu vingi vya kwetu na siyo kutegemea Mataifa mengine.
Naye Makamu mkuu wa chuo cha Dar es salaam (UDSM) Profesa William anangisye amesema kuwa chuo hicho kimekuwa na taratibu za kutenga bajeti kwa ajili ya utafiti ambapo kwa mwaka 2021/22 imetengwa zaidi ya bilioni 2 kwa ajili ya tafiti ambapo tafiti hizo ni kwa ajili ya kueleKea katika kutatua matatzo ya wananchi.
Amesema chuo hicho kimekuwa pia kikitenga fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kununua vifaa na kufanya tafiti huku akidai changamoto kadha bado zinaikabili chuo hicho.