|
Mgeni Rasmi, Ofisa Elimu wa Mkoa wa Mara, Bw. Benjamin Oganga (kulia) akimuwakilisha Katibu Mkuu TAMISEMI akipata maelezo kwenye Banda la Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) kwenye hafla ya kufunga Maadhimisho ya Juma la Elimu kitaifa yaliofanyika wilayani Rorya-Shirati. |
|
Mgeni Rasmi, Ofisa Elimu wa Mkoa wa Mara, Bw. Benjamin Oganga (wa nne kulia) akipata maelezo kutoka Banda la Sense International kwenye hafla ya kufunga Maadhimisho ya Juma la Elimu kitaifa yaliofanyika wilayani Rorya-Shirati. Kutoka kulia ni Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga, Mkurugenzi wa Shirika la CAMFED, Lydia Wilbard ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya TEN/MET pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TEN/MET, Dk. John Kalage wakiongozana na mgeni rasmi. |
|
Mgeni Rasmi, Ofisa Elimu wa Mkoa wa Mara, Bw. Benjamin Oganga (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka Banda la CAMFED kwenye hafla ya kufunga Maadhimisho ya Juma la Elimu kitaifa yaliofanyika wilayani Rorya-Shirati. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TEN/MET, Dk. John Kalage na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Rorya, Gerald Ng’ong’a (wa tatu kulia) wakiongozana na mgeni rasmi. |
|
Mgeni Rasmi, Ofisa Elimu wa Mkoa wa Mara, Bw. Benjamin Oganga (wa tatu kulia) akipata maelezo kutoka Banda la Shule Direct kwenye hafla ya kufunga Maadhimisho ya Juma la Elimu kitaifa yaliofanyika wilayani Rorya-Shirati. Kutoka kulia ni Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga na Mwenyekiti wa Bodi ya TEN/MET, Dk. John Kalage wakiongozana na mgeni rasmi. |
|
Mgeni Rasmi, Ofisa Elimu wa Mkoa wa Mara, Bw. Benjamin Oganga (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka Banda la UWEZO Tanzania kwenye hafla ya kufunga Maadhimisho ya Juma la Elimu kitaifa yaliofanyika wilayani Rorya-Shirati. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TEN/MET, Dk. John Kalage wakiongozana na mgeni rasmi. |
|
Mgeni Rasmi, Ofisa Elimu wa Mkoa wa Mara, Bw. Benjamin Oganga (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka Banda la Haki Elimu kwenye hafla ya kufunga Maadhimisho ya Juma la Elimu kitaifa yaliofanyika wilayani Rorya-Shirati. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TEN/MET, Dk. John Kalage wakiongozana na mgeni rasmi. |
|
Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga (kulia) akizungumza kwenye hafla ya kufunga Maadhimisho ya Juma la Elimu kitaifa yaliofanyika wilayani Rorya-Shirati. |
|
Mwenyekiti wa Bodi ya TEN/MET, Dk. John Kalage (katikati) akizungumza kwenye hafla ya kufunga Maadhimisho ya Juma la Elimu kitaifa yaliofanyika wilayani Rorya-Shirati. Wa pili kulia ni Mgeni Rasmi, Ofisa Elimu wa Mkoa wa Mara, Bw. Benjamin Oganga na Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga (kulia) wakifuatilia. |
|
Mgeni Rasmi, Ofisa Elimu wa Mkoa wa Mara, Bw. Benjamin Oganga akimzawadia mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi wilayani Rorya aliyefanya vizuri ikiwa ni sehemu ya kuwamotisha wanafunzi wengine kufanya vizuri zaidi kwenye hafla ya kufungwa kwa Maadhimisho ya Juma la Elimu kitaifa yaliofanyika wilayani Rorya-Shirati. |
|
Mgeni Rasmi, Ofisa Elimu wa Mkoa wa Mara, Bw. Benjamin Oganga akimzawadia mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari wilayani Rorya aliyefanya vizuri ikiwa ni sehemu ya kuwamotisha wanafunzi wengine kufanya vizuri zaidi kwenye hafla ya kufungwa kwa Maadhimisho ya Juma la Elimu kitaifa yaliofanyika wilayani Rorya-Shirati. |
Na
Mwandishi Wetu, Rorya-Tarime
MTANDAO wa
Elimu Tanzania (TEN/MET) umechangia fedha zaidi ya shilingi milioni 30.9
kugharamia miundombinu ya elimu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Juma la Elimu
Kitaifa (The Global Action Week for Education – GAWE) lililofanyika wilayani
Rorya Mkoa wa Mara.
Akizungumzia katika hafla ya kufungwa kwa maadhimisho
hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya TEN/MET, Dk. John Kalage amesema mchango huo ni wa
fedha tasilimu na wadau hao pia kushiriki katika shughuli za kijamii
kuhamasisha wananchi kujitolea na kutoa motisha kwa wanafunzi wanaofanya vizuri.
Alisema wadau hao wa elimu katika juma la elimu
wameshiriki kusomba vifaa vya ujenzi na mafundi, kufyatua
matofari katika shule ya msingi Obwere wilayani humo, ikiwa ni kuhamasisha
wanajamii kujitolea kwenye shughuli za ujenzi wa miundombinu ya elimu.
Akifafanua zaidi mchango wao, wa kuacha alama za
maadhimisho amesema wadau wa TEN/MET
wamefanikiwa kuchangia fedha taslimu shilingi milioni 17.4 Ili kuendeleza
utamaduni kuacha alama na kuunga mkono jitihada za jamii na Serikali katika
kuboresha elimu.
“…Mtandao wa Elimu Tanzania kwa
kushirikiana na mashirika wanachama walioshiriki katika maadhimisho haya,
tumeshirikiana na jamii katika shughuli mbalimbali zinazolenga kuboresha miundombinu
kwenye shule tulizotembelea kama vile usombaji wa vifaa vya ujenzi na kuungana
na mafundi kufyatua matofari katika shule ya msingi Obwere.
“TEN/MET kupitia wanachama wake
itachangia fedha taslimu shilingi million 17 na laki nne, Kwa mchanganuo ufuatao;
Tshs milioni 8 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi darasa shule ya msingi Obwere
wilayani Rorya.
Tunatoa mabati 100, yenye thamani ya shilingi
milioni 3.2 kwa ajili ya kupaua jengo la bweni la Shule ya Sekindari ya Prof.
Sarungi litakalochukuwa wanafunzi wa kike 80, Tunachangia shilingi milioni 3 kwa
Shule ya Sekondari Bukama ili kukamilisha ujenzi wa jengo la maabara, na Shule
ya Msingi Utegi tutachangia Mabati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 3.2,” alisema Dk. Kalage.
Aidha alibainisha kuwa, TEN/MET pia imewazawadia
baadhi ya wanafunzi T-shirts, madaftari na chupa za kunywea maji, vifaa vyote
kwa pamoja vikiwa vimegharimu zaidi ya shilingi milioni 13 na elfu 54 ikiwa ni
kuleta motisha kwa wanafunzi kufanya vizuri na kuchochea mafanikio ya elimu
eneo hilo.
Hata hivyo, aliongeza kuwa wadau wa
Mtandao wa Elimu kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri pia waliendesha
harambee na kupata kiasi cha shilingi 500,000 kwa ajili ya kuhudumia watoto
wenye ulemavu katika Shule ya Msingi Utegi, Kati ya hizo shilingi 100,000 itatumika
kumhudumia msichana mwenye mahitaji maalum wa Shule ya Sekondari Bukama.