KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii ikipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),Dk.Maulidi Banyani,mara baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba 300 katika eneo la Iyumbu na nyumba 100 wilayani Chamwino zilizojengwa na Shirika hilo leo June 3,2021 Mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii ,Dkt.Aloyce Kwezi,akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba 300 katika eneo la Iyumbu na nyumba 100 wilayani Chamwino zilizojengwa na Shirika la NHC leo June 3,2021 Mkoani Dodoma.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Lukuvi,akizungumza na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii pamoja na watendaji wa NHC mara baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba 300 katika eneo la Iyumbu na nyumba 100 wilayani Chamwino zilizojengwa na Shirika la NHC leo June 3,2021 Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula,,akizungumza na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii pamoja na watendaji wa NHC mara baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba 300 katika eneo la Iyumbu na nyumba 100 wilayani Chamwino zilizojengwa na Shirika la NHC leo June 3,2021 Mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),Dk.Maulidi Banyani,akitoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii ambayo imefanya ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba 300 katika eneo la Iyumbu na nyumba 100 wilayani Chamwino zilizojengwa na Shirika hilo leo June 3,2021 Mkoani Dodoma.
Mkurugenzi wa Uhandisi na Ujenzi wa NHC,Haikamen Mlekio akizungumzia shughuli zinazofanyika katika maeneo yote mawili Chamwino na Iyumbu kwa kununua mashine 17 za kutengeneza matofali ambazo zimeajiri vijana 60 ambao wana uwezo wa kutengeneza matofali 20,000 baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba 300 katika eneo la Iyumbu na nyumba 100 wilayani Chamwino zilizojengwa na Shirika hilo leo June 3,2021 Mkoani Dodoma.
Mhandisi anayesimamia Ujenzi wa nyumba Chamwino Grace Msita,akizungumzia nyumba hizo zinajengwa katika ubora wa hali ya juu ambapo madini ya ujenzi kama kokoto, mawe na mchanga vinapimwa ubora wake katika maabara ya Tarura kabla ya kutumika baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba 300 katika eneo la Iyumbu na nyumba 100 wilayani Chamwino zilizojengwa na Shirika hilo leo June 3,2021 Mkoani Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii (waliokaa)pamoja na watumishi wa shirika la NHC waliosimama wakifatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba 300 katika eneo la Iyumbu na nyumba 100 wilayani Chamwino zilizojengwa na Shirika hilo leo June 3,2021 Mkoani Dodoma.
Mhandisi anayesimamia Ujenzi wa nyumba Chamwino Grace Msita,akionyesha mchoro wa ramani wa nymba zinazojengwa Chamwino wakati wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba 300 katika eneo la Iyumbu na nyumba 100 wilayani Chamwino zilizojengwa na Shirika hilo leo June 3,2021 Mkoani Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii wakiendelea kukagua ujenzi wa nyumba 300 katika eneo la Iyumbu na nyumba 100 wilayani Chamwino zilizojengwa na Shirika la NHC leo June 3,2021 Mkoani Dodoma.
Mafundi wakiendelea na kasi ya ujenzi wa nyumba za NHC zinazojengwa Chamwino.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula,akishiriki kumwanga zenge wakati wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba 300 katika eneo la Iyumbu na nyumba 100 wilayani Chamwino zilizojengwa na Shirika la NHC leo June 3,2021 Mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),Dk.Maulidi Banyani,akishiriki kumwanga zenge wakati wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba 300 katika eneo la Iyumbu na nyumba 100 wilayani Chamwino zilizojengwa na Shirika la hilo leo June 3,2021 Mkoani Dodoma.
Muonekano wa nyumba zinazojengwa Chamwino.
Mkurugenzi wa Uhandisi na Ujenzi wa NHC,Haikamen Mlekio,akionyesha mchoro wa ramani wa nymba zinazojengwa Iyumbu wakati wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba 300 katika eneo la Iyumbu na nyumba 100 wilayani Chamwino zilizojengwa na Shirika hilo leo June 3,2021 Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,Mwalimu Josephat Maganga,akizungumza na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba 300 katika eneo la Iyumbu na nyumba 100 wilayani Chamwino zilizojengwa na Shirika la NHC leo June 3,2021 Mkoani Dodoma.
……………………………………………………………………………..
Na Alex Sonna,Dodoma
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii imelipongeza Shirika la Nyumba (NHC) kwa kutekeleza miradi yenye ubora zikiwemo nyumba 400 zinajengwa Mkoani Dodoma.
Hayo yameelezwa leo,June 3, 2021 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Dkt.Aloyce Kwezi wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba 300 katika eneo la Iyumbu na nyumba 100 Wilayani Chamwino zilizojengwa na Shirika hilo.
Mwenyekiti huyo,amesema Kamati hiyo imeridhishwa na ujenzi wa nyumba hizo huku akimpongeza Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi (William Lukuvi) na Watendaji wa Shirika hilo kwa kuweza kusimamia vizuri ujenzi wa nyumba hizo.
“Nimeona miradi ya National Housing (NHC) inayoendelea karibu nyumba 1000 kwa awamu zote tatu,miradi hii kwa kweli inatakiwa kupongezwa ndio maana kamati yangu,imeanza kumpongeza Waziri kwa kazi nzuri na kuwapongeza watendaji wake kwani nimeona ubora wa miradi inayoendelea.
Mwenyekiti huyo amesema ujenzi wa nyumba hizo ni shamba darasa kwa wajenzi binafsi pamoja na wajenzi wengine ambao wanaendelea kujenga nyumba Jijini Dodoma.
“Kwanza ni ubora lakini la pili miradi hii ni shamba darasa kwa wajenzi wabinafsi pamoja na wejenzi wengine ambao watapenda kwa ajili ya kuikuza Dodoma yetu,lakini tutafurahi zaidi kwa sababu lengo ni miradi ikamilike kwa wakati halafu wananchi waje wapate huduma.
“Wananchi wengi hapa ni wageni wanahitaji nyumba lakini nyumba hapa zinauzwa kwa bei ambayo tunaona inaenda kuwa nzuri niipongeze sana Wizara kwa usikivu wao kwa kuweza kusikiliza maoni ya kamati,”amesema.
Kwa upande wake,Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Lukuvi amesema wanajenga nyumba za Apatment 100 Chamwino pamoja na zile ambazo zinajitegemea 300 katika eneo la Iyumbu Mkoani Dodoma ambazo zitakopeshwa kwa wananchi ikiwemo wafanyakazi wa Serikali.
“Na NHC inayotumia mradi huu kama shamba darasa kuwafundisha Real Estate namna bora ya kujenga nyumba imara bora lakini pia kumekuwa na udhaifu kwa wauzaji wa nyumba ambao wamekuwa wakifanya udanganyivu kwa kuwauzia nyumba matokeo yake wafanyakazi wanalipa ya muda mrefu,”amesema.
Amesema kwa mara ya kwanza Serikali inataka kuonesha mkopaji anatakiwa kupewa siku za kutosha kuweza kulipa mkopo wa nyumba hizo.
“Kwa hiyo NHC tunataka kuwafundisha kwa vitendo,tutakabidhi nyumba kwa mnunuzi siku atakayolipia zitakapokwisha siku atakayolipia nyumba hii kwanza sisi tutamsaidia kupatikana kwa mkopo wa kununua nyumba hiyo,”amesema.
Waziri Lukuvi amesema Serikali itamsaidia mnunuzi wa nyumba aweze kupata mkopo benki wa nafuu ambao hautakuwa mgumu kwake kulipa.
“Kila mnunuzi wa nyumba hizo Serikali tutamsaidia kupata mkopo kwa Benki kwa gharama nafau lakini pili siku atakayolipa nyumba hii ndio siku atakayopata hati ya kumiliki lakini atapata funguo ya nyumba ili mnunuzi wa nyumba hizi tunataka siku atakayotransfer fedha NHC ndio siku ambayo atakabidhiwa funguo aingie ndani ya nyumba na kupewa hati ya kumiliki nyumba hiyo,”amesema.
Waziri Lukuvi amesema mpango wa Serikali ni kujenga nyumba katika kila eneo katika Mikoa hapa nchini.
“Sisi Shirika la nyumba kwetu sisi kama Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa sekta ya nyumba tumeiteua Shirika la Nyumba kama kiongozi wa wajenzi wa nyumba hizi za makazi.
“Kwa hiyo hawa wanapashwa sio kupangisha tu nyumba lakini ni kiongozi wa kuonesha mfano namna ya ujenzi wa nyumba bora zinavyotakiwa kujengwa nyumba za gharama nafuu lakini na utaratibu ulionafuu kwa wananchi,”amesema.
Alipoulizwa iwapo nyumba hizi zikanunuliwa na Mfanyabishara mmoja ,Waziri Lukuvi amesema Serikali kipaumbele chake ni wafanyakazi wa Serikali na hawatakuba, jambo hilo litokee kwani Serikali imetoa fedha kwa ajili ya watu maskini.
“Kwa kweli hatutaruhusu kununua nyumba zaidi ya moja na tutawajua tu hatutaki nyarubanya hapa kwamba ununue zote halafu upangishe watu wote haiwezekani kwanza Seriakli imetoafedha hizi ili mwananchi akopshwe kwa gharama nafuu,”amesema
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba(NHC),Dkt.Maulidi Banyani amesema dhamira yao ni kujenga miradi mingi nchini lakini akadai ni lazima wawe na ardhi ya kutosha.
“Sisi kama NHC yapo maeneo mbalimbali nchini tunadhamiria kujenga miradi ya namna hii ili tuweze kufanikisha haya ni lazima tuwe na ardhi na sisi kwa hivi sasa tuna ardhi katika maeneo mbalimbali kwa mfano, Mtwara,Mara,Lindi,”amesema.
Amesema kwa Mkoa wa Dodoma wamefanya mazungumzo na Jiji la Dodoma na tayari wameishapata maeneo Mapinduzi na Mahoma kwa ajili ya awamu ya pili ya ujenzi wa nyumba maalum za viongozi
“Kwa hiyo tumejiandaa na tunahakika kwamba miradi hii itaendelea kutekelezwa sehemu mbalimbali za Nchi,”amesema.