Naibu waziri wa afya , maendeleo ya jamii .wazee ,jinsia watoto na watu wenye ulemavu,Dkt. Godwin Mollel akizungumzia na waandishi wa habari mjini Arusha .
*************************************
Happy Lazaro, Arusha
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia, Watoto na watu wenye ulemavu, Dkt. Godwin Mollel amewataka wataalamu wa mifumo ya Tehama katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro kutengeneza mfumo utakao wawezesha wageni wanao ingia nchini kufanya malipo ya vipimo vya Korona kabla hawaja fika nchini hali itakayo wapunguzia muda wa kukaa uwanjani hapo.
Dokta Mollel ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha ambapo amesema kuwa,mfumo huo wa Tehama utawasaidia watoa huduma za afya kutoa huduma za afya kwa wepisi kutokana na kuwa na taarifa mapema za wageni wanao wasili nchini kupitia kiwanja hicho.
Aidha Mollel amewataka watoa huduma za afya katika kiwanja cha ndege cha kimataifa KIA kufuata sheria kanuni na taratibu za Afya zilizo wekwa na Wizara ya Afya pamoja na zile za shirika la Afya Duniani, WHO.
Aliwataka wafanyakazi wanaotoa huduma za afya katika viwanja hivyo na mipakani wasitoke nje ya viwango vya shirika la Afya ,wahakikishe wanawahudumia watu wengi kwa wakati mmoja ili kusiwepo na msongamano katika eneo hilo.
Alifafanua kuwa,endapo wageni watalipia fedha hizo kabla ya kufika uwanja wa ndege itarahisha Sana utoaji wa huduma kwa haraka na kupunguza swala la kucheleweshwa kwa wateja kwani kuna umuhimu mkubwa tukatengeneza mazingira ambayo mgeni alipe hela huko huko ili wakifika uwanjani wasikae zaidi dakika 30 kila kitu kiwe kimeisha.
“Nimeiomba timu ya Afya ya mkoa wa Kilimanjaro waje na ushauri wa kuhakikisha tunaboresha huduma kuondoa hizo kero,kwani tukijipanga na watu wa afya wa Kilimanjaro ili waweze kutoa wataalamu waje kushirikiana na wenzao wa afya ili huduma iende kwa haraka zaidi.”amesema Dokta Mollel.
Alifafanua kuwa,kuhusu swala la maelekezo ya masaa 72 kwa wageni wanaosafiri wataenda kuliangalia watapanga na kukutana na wadau wa utalii ,tatizo hili kwenye nchi yetu wamedhibiti wanataka kuhakikisha wenzetu waliopo nje hawaleti tatizo toka nje ,kwani kuna wageni wengine hata kabla hawajafika masaa 72 yanakuwa yameisha watakutana na wenzao wakae waje na njia ambao haitawasumbua wageni wao.
Aidha Dokta Mollel aliongeza kuwa,wanataka kuwasiliana na wenzao wa Zanzibar kutengeneza utaratibu uliofanana unaowafanya wote waende pamoja.
Aidha alizitaka mamlaka husika ,kurahisisha mazingira ya wafanyabiashara na watu wetu wanaposafiri kufanya biashara maeneo mbalimbali na watu waridhike na huduma wanazopewa.
“Tunataka watu waliopo viwanja vya ndege ama kwenye mipaka yetu wabebe sura ya nchi kwa wageni wetu kwani huduma watakazotoa ndo zinapeleka picha ya nchi yetu na sisi tukoje hivyo uzalendo wa hali ya juu unatakiwa”amesema.
Dokta Mollel aliwataka watu wote wanaohusika kwenye viwanja na mipaka kushirikiana kwa pamoja katika kuwasikiliza vizuri wageni wao na kutatua changamoto zao kwa haraka ili waweze kuitangaza nchi yao wanakapokuwa.