Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ametembelea banda la Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya 2021 katika Viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma. Kauli mbiu katika maonesho hayo mwaka huu ni “Kuimarisha ushirikiano wa wadau katika kukuza ujuzi kwa maendeleo ya Uchumi wa Viwanda”.
Mkuu wa Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Naibu Kamishna (DCF) Kennedy Komba akimkabidhi zawadi ya kizimia moto cha huduma ya kwanza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa baada ya kupata maelezo ya namna ya kutumia kifaa hicho wakati alipotembelea banda la Chuo hicho katika Viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma. Kauli mbiu katika maonesho hayo mwaka huu ni “Kuimarisha ushirikiano wa wadau katika kukuza ujuzi kwa maendeleo ya Uchumi wa Viwanda”.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea kizimia moto cha Fire Blanket kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Naibu Kamishna (DCF) Kennedy Komba wakati alipotembelea banda la Chuo hicho katika Viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma. Kauli mbiu katika maonesho hayo mwaka huu ni “Kuimarisha ushirikiano wa wadau katika kukuza ujuzi kwa maendeleo ya Uchumi wa Viwanda”. (Picha Zote na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
**************************
DODOMA 28 MEI, 2021
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ametembelea banda la Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya 2021 katika Viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Mhe. Waziri Mkuu alipata fursa ya kupata elimu ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto kwa kuelekezwa jinsi vifaa mbalimbali vinavyoweza kutumika kuzuia moto katika majengo mbalimbali.
Akiambatana na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhe. Prof. Joyce Ndalichako kwa pamoja walipata nafasi ya kumsikiliza Mkuu wa Chuo hicho Naibu Kamishna (DCF) Kennedy Komba aliyekuwa akielekeza jinsi vifaa hivyo vinavyofanya kazi.
Mhe. Waziri Mkuu aliuliza swali akitaka kujua Jeshi hilo limejipangaje kukabiliana na matukio ya moto yanayoendelea katika shule mbalimbali hapa nchini.
Akijibu swali hilo Mkuu wa Chuo DCF Komba alisema “tumeingia makubalianao na Chama cha Skauti Tanzania ili tushirikiane nao kwa kutoa elimu, na tayari tumeshaanza kutoa elimu katika shule zetu kwa kushirikiana na Chama cha Skauti njia hii itasaidia kupunguza majanga ya moto katika shule zetu” alimaliza Mkuu wa Chuo.
Mkuu wa Chuo alimaliza kwa kumkabidhi zawadi ya vizimia moto vya huduma ya kwanza Mhe. Waziri Mkuu ambavyo ni portable fire extinguisher na fire blanket.