Mwenyekiti wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) ngazi ya Makatibu Wakuu, ambaye pia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Afrika Mashariki kutoka Kenya, Dkt. Kevit Desai akiongea na wajumbe wa mkutano ulifanyanyika leo Jijini Arusha
Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara na Mkuu wa Ujumbe wa Tanzania, Bw. Doto James akifafanua jambo katika mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki sekta ya biashara, viwanda, fedha na uwekezaji (SCTIFI) ulifanyanyika leo Jijini Arusha. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Prof. Godius Kahyarara na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban.
Ujumbe wa Burundi ukifuatilia mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki sekta ya biashara, viwanda, fedha na uwekezaji (SCTIFI) ulifanyanyika leo Jijini Arusha.
Ujumbe wa Kenya ukifuatilia mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki sekta ya biashara, viwanda, fedha na uwekezaji (SCTIFI) ulifanyanyika leo Jijini Arusha.
Baadhi ya wajumbe wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki sekta ya biashara, viwanda, fedha na uwekezaji (SCTIFI) leo Jijini Arusha. Wajumbe wakifuatilia mkutano
****************************
Na Mwandishi wetu, Arusha
Baraza la Mawaziri la kisekta la Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili wanategemea kukutana kesho tarehe 28 Mei 2021 Jijini Arusha kujadili masuala mbalimbali ya kukuza biashara na uwekezaji ndani ya Jumuiya hiyo.
Mkutano huo wa Mawaziri umetanguliwa na mkutano wa Makatibu Wakuu wa sekta ya Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) wa Jumuiya hiyo uliofanyika leo jijini Arusha ambapo pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamepokea na kujadili ripoti mbalimbali ikiwemo ripoti za baraza la kisekta la mawaziri wa fedha, ripoti ya kamati ya forodha, ripoti ya kamati ya biashara, ripoti ya kamati ya viwango ya Afrika Mashariki, ripoti juu ya masuala ya ushindani pamoja na ripoti ya kamati ya uwekezaji.
Mkutano wa Makatibu Wakuu wa leo tarehe 27 Mei 2021 utafuatiwa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa kisekta tarehe 28 Mei 2021 jijini Arusha.